Achraf Hakimi: Mmoja kati ya 'full backs' bora kabisa ulimwenguni wanaochipukia

Joined
Dec 9, 2018
Posts
66
Reaction score
52
Borussia Dortmund ni moja ya timu zilizowahi kuwa na full backs bora kabisa. Moja kati ya full backs wa Dortmund ni Lukasz Pisczek ambaye amekuwa klabuni hapo tangu 2010 akiwa katika ubora wa hali ya juu.

Beki huyu kutoka Poland alikuwa bora sana katika ukabaji pamoja na kupandisha mashambulizi kama modern football ianawataka mabeki wengi wa pembeni kucheza.Umri ukiwa umemtupa mkono Mpolish huyu Borussia Dortmund wanaonena kupata mbadala sahihi. Kijana wa Kimorocco mwenye uwezo mkubwa kabisa, Achraf Hakimi ambaye wenyewe wanapendelea kumuita 'a flying Moroccan' maana yake Mmorocco anayepepea.

Kijana huyu alizaliwa nchini Hispania na wazazi wa Kimorocco katika jiji la Madrid.Baada ya kuonesha mapenzi yake katika mchezo wa soka, alijiunga na klabu ya CD Colonia kisha kuchukuliwa na akademi ya Real Madrid.

Alipandishwa timu ya wakubwa mwaka 2017 kumsaidia Dani Carvajal kwenye mbavu ya pembeni.Japokuwa hakupata sana nafasi ya kuingia katika kikosi cha kwanza cha the Los Blancos,alifanikiwa kuwa Mmoroccoo wa kwanza kushinda taji la UEFA Champions League akiwa na Real Madrid mwezi May, 2018 ambapo aliitumikia klabu hiyo katika mechi mbili.

Baada ya kukosa muda wa kutosha kucheza katika kikosi cha kwanza cha Real Madrid alipelekwa kwa mkopo wa miaka miwili katika klabu ya Borussia Dortmund. Baada ya kufanikiwa kuingia katika kikosi cha kwanza cha Dortmund, amefanikiwa kuwa moja kati ya mabeki bora kabisa ulimwenguni akiwa na miaka 21 tu.

Ana uwezo mkubwa wa kukaba,kupandisha timu na hata kufunga sio shida kwake.Amewaokoa Dortmund Mara nyingi wasipate vichapo kutokana na magoli yake. Magoli mengi yanayofungwa na kina Marco Reus pamoja na Parco Alcacer pale Borussia Dortmund yana mchango mkubwa sana wa huyu kinda.Anapiga krosi nzuri zenye macho na ana uwezo mkubwa sana wa kukokota mpira (dribbling).

Magoli mengi ya Dortmund chini ya kocha Lucien Favre yana mchango mkubwa sana wa huyu Mmorocco.

Mwaka 2018 alifanikiwa kuvhukua tuzo ya mchezaji bora chipukizi kutoka Africa na mwaka huu pia yupo katika nominees wa hiyo tuzo.

Binafsi namuona huyu kinda mbali sana baada ya miaka kadhaa.Muda unapewa jukumu lingine kubwa zaidi la kutoa ushahidi juu ya hili.Tusubiri tuone.

----Bobvin's thought----
Adios Amigo
 
Pamoja na ubora wake jana La pulga alikua anakatiza katikati yao kama sungura dortimond walikua wanamfuata wanne wanne......
King messi acha kabisa..
 
Mkuu huyu dogo ana uwezo wa kucheza right & left wings,central defender na hata kama winga
 
Arudishwe Benabeu. Ameshakwiva kurejea kwa chama langu Madrid.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…