Achukue hatua gani ili apate haki yake?

The GT

JF-Expert Member
Joined
Apr 15, 2015
Posts
461
Reaction score
529
Umofia kwenu,

Kuna rafiki yangu yeye anafanya biashara ya kukopesha fedha kwa watumishi wa umma kwa marejesho ya muda mfupi isiyozidi miezi 4 akitumia mikataba fulani anayodhani ina security kwake na mteja kuacha kadi ya bank.

Ishu ilivyo sasa kuna mteja wake wa muda mrefu ambaye mara ya mwisho amemkopesha hela kwa kuaminiana tu kwa kumtumia kwenye simu bila kumjazisha huo mkataba na ni mwezi wa pili huu sasa hajamrejeshea pesa yake.

Ushaidi aliobakiwa nao ni wa kadi ya bank ambayo nayo haifanyi kazi kwa sasa na pia ana SMS anayoamini ina ushahidi ambayo mteja wake akiomba aanze kumlipa mwezi huu baada ya mwezi wa kwanza kushindwa kurejesha na hivi sasa mawasiliano na huyo mteja hayapatikani vizuri akiamini mteja wake amemtapeli.

Kipi afanye huyu swahiba ili apate haki yake? Yeye anawaza kumpeleka mahakamani mdeni wake.
 
Kadi ya bank haiwezi kuwa ushahidi nadhani, jamaa anakopesha kiholela mno.
Mtu anakuachia kadi kisha anaenda bank anasema kadi imepotea inakuwa blocked anapewa nyingine.
Yani kadi ya bank haiwezi kuwa ushahidi maana bank hairuhusu mtu mwingine asiye mwenye account kupewa kadi.
 
Na nahis yeye paia anvunja sheria,,kufanya biashara bubu bila kulipa kodi,,,, akijipeleka hawata muacha salama hasa kwa zama hizi za ukiuza dai Risit
 
Katika accounts kuna kitu ki nacho itwa "bad debts" bora kukubari matokeo na aendelee na biashara za ke
 
Nyie mnaokopesha kwa dizaini hii hamlipi kodi halafu mnatoza riba kubwa mnachangia kuwafanya watanzania maskini zaidi ya walivyo.

Nakushauri ukareport police ili useme vizuri inakuwaje unamiliki kadi ya mtu mwingine, kama sio wizi huo ni nini.
 
Hivi mtaacha lini kusingizia matatizo yenu kwa wengine?wewe umetapeliwa,kuwa muwazi upewe msaada,kama umeliwa umeliwa tu hamna namna,mambo ya kusema kuna rafiki yangu sijui jirani yangu....pambaf.
 
Ndugu Nelson nely kwa comment hiyo ndiyo uwepo wako unaofanya dunia ikamilike,okay tufanye ndiyo mimi nimetapeliwa,nipe msaada wako sasa.
 
Kapigwa Huyo tena kizamaaani aongee na Jamaa. maana ishakua kesi ya kibaharia wamalizane kibaharia haina kwenda polisi wala mahakamani,
 
Hiyo ni biashara haramu ambayo sheria haziwezi kukusaidia . Ni kama ufanye biashara ya bangi afu mwenzako kakuzurumu uende mahakamani au polisi kudai malipo yako ya bangi.

Huwa nacheka sana mtu anakukopesha kwa riba na vimikataba hewa ambavyo havina nguvu kisheria sema tu watu huwa wanarudisha kwa kujali ubinadamu.

Biashara halali ni ile utakayokuwa umeisajili kisheria na unalipa kodi ya serikali hapo akikuzurumu una haki ya kumshitaki .
 
Sio kweli unless umekutana na ambao hawajui kuandika mkataba, kwanza ujue kiujanja mtu anayefanya biashara hiyo anatambuliwa kama individual money lender ambayo ni informal way of microfinance... Sasa kinachofanyika mkataba hauandikwi kwamba umempa kiasi hiki arudishe kiasi hiki na riba hii hapo utapigwa kweupeee ila mkataba wa aina hii huandikwa tu nimemkopesha kiasi hiki atarejesha muda fulani... Nimefanya hii ishu na shahidi yangu alikua mwenyekiti wangu wa mtaa na mhuri wake kabisa...so hii ukiifanya kiboya unakalia kucha ila ukiwa mzoefu ni bonge moja la biashara la kuwala maboya
 
Atafute beberu jeupe kisha amuulize Mshana Jr taratibu za kiasili za kumshawishi mdeni arudishe amana haraka bila usumbufu
 
kwanza atambue kuwa KISHERIA individual person haruhusiwi kukopesha pesa kwa riba whatsoever. kwa sababu hajasajiliwa kama taasisi ya kifedha ili awe na uwezo huo. kwa maana nyingine kunaposibility akapoteza hiyo kesi mahakaman kama atataka kupeleka huko. ila pia kuna altenative nyingine ambayo anaweza akatumia kuipata pesa yake kwa mfumo huo huo wa sheria and it is the only available option naweza kusema kwa upande wangu. unless otherwise tutaftane for more infos au kama ana wakili karibu amfate ape msaada wa kisheria.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…