Aende mahakamani haraka#HABARI Mwanamke mmoja jijini Dar es Salaam aliyefahamika kwa jina Gift Mtanda, amekumbwa na mkasa mkubwa baada ya nyumba yake kupigwa mnada kufuatia mkopo wa benki alioudhamini kwa rafiki wa familia.
Inadaiwa kuwa nyumba hiyo iliwekwa dhamana benki ili kumsaidia rafiki huyo kupata mkopo, lakini baadaye alishindwa kurejesha fedha hizo, hali iliyosababisha hatua za kisheria kuchukuliwa dhidi ya mdhamini.
Akizungumzia tukio hilo, Gift amesema mabaunsa walifika nyumbani kwake asubuhi ya Machi 25, 2026 na kuanza kutoa vitu vya ndani ya nyumba wakidai wametumwa na benki.
Akieleza kuwa tukio hilo lilimshtua na kumuumiza sana kwa kuwa yeye hakuwa mkopaji moja kwa moja, bali alimdhamini rafiki wa familia ambaye alishindwa kulipa deni, na hivyo kusababisha nyumba yake kupigwa mnada kufidia mkopo huo. #EastAfricaTV
Mahakama haiwezi kumsaidia kitu. Mali yake ndiyo ilikuwa dhamana ya mkopo.Aende mahakamani haraka
Yes mdhamini anaweza kuweka dhamana itumike kama collateralNi kwamba mdhamini naye huwa anatakiwa kuweka mali yake kama security?
Abla hotel and apartments zimekwenda huku mwenyewe mu Oman akiangaliaWhat a big mistake.. Huo unaitwa wema wa mshumaa
Ukiwa na shida na pesa halafu unaiona hiyo hapo mbele yako, Hilo hulikumbuki kabisa yaaniPole yake,
Siku zote kabla ya kufanya jambo lolote lile au kuchukua maamuzi yeyote yale,
Ni vizuri zaidi ukalijua jambo hilo kwa undani zaidi na kujua matokeo yake ya baadae kama mambo hayatakwenda kama inavyo tarajiwa.
Abla hotel and apartments zimekwenda huku mwenyewe mu Oman akiangalia
Huyo mama ni mjinga, hajui kua unapomdhamini mtu ina maana unachukua kila kitu kwa lolote litakalomtokea uliemdhamini.Kwahio hapo imekula kwake wana haki ya kuichukua hio nyumba yake. Watu wajifunze hapo. Ndio maana halisi ya mdhamini = Guarantor.