ACt nguvu yao ya kuendelea kuwepo iko Zanzibar,haswa Pemba, na wao ajenda yao kubwa ni serikali tatu, nje ya ajenda hiyo wanzibar hawatakuelewa.Maalim Seif alikuwa na nguvu kisiasa lakini serikali 3 zilimzuia kwenda Ikulu hadi akaondoka zake. Nyie mna mikakati Gani tofauti na Seif?
Kushinda sio kazi ila kazi ni kutangazwa, Shauri mjaribu kuhubiri serikali 1 au 2 hizihizi hadi hapo mtakapokwenda Ikulu kwa kutumia Katiba hiihii ya serikali 2. Msidhani akina Jecha wamekufa wote.
Tanzania Kuna watu wasiojulikana ambao wanailinda Katiba hii dhidi ya mtu yeyote hata awe nani atakaeivunja au mwenye mwelekeo wa kuivunja, Watakukalisha chini tu utake usitake. Kumbuka kuwa hata Rais wa Katiba pia analindwa kama inavyolindwa Katiba na Jamhuri. Hata CDF, jaji Mkuu na spika nao wanalindwa kama wengine tu, ni mfumo wa kuilinda Katiba na mipaka ya nchi dhidi ya adui wa ndani na nje.ACt nguvu yao ya kuendelea kuwepo iko Zanzibar,haswa Pemba, na wao ajenda yao kubwa ni serikali tatu, nje ya ajenda hiyo wanzibar hawatakuelewa.
Na sasa wana advantage kubwa Rais wa JMT ni Mzanzibar asilia. Na hiyo ni kete muhimu sana kwao wakiitumia vyema, huko nyuma 1984 Marehemu Aboud Jumbe alijaribu kudai mabadiliko kwenye muundo wa Muungano na ilimgharimu urais wa Zanzibar na umakamu wa JMT.
Na inawezekana ndio maana alipendekezwa Mzee Mwinyi kurithi nafasi yake,ambaye historia yake inaonekana alizaliwa Pwani Mkurunga na ndiko babake inasemekana ndiko alikozikiwa,kwa hiyo hata uzanzibar wake nakumbuka ulitiliwa shaka.
Kama kuna fursa nzuri Kwa wazenji ni sasa. ACT wakikomaa nayo haitakuwa ngumu kuipata.
Kumbuka hata huyu mgombea mwenza wa ACT Othman Masoud,aliwahi kuwa AG wa Zanzibar, na yeye ndiye aliikataa katiba pendekezwa wazi kwenye bunge la katiba,na haikuhitaji kura ya siri kama wengine kwenye bunge la katiba na msimamo huo ndio ukimuondoa kwenye nafasi ya uAG Zanzibar.
Na wewe toka Samia ashike dola umewahi kumsikia akimkosoa pamoja na kuwa upinzani? Za kuambiwa changanya na zako.
Kwamba huu Muungano ni imara kuliko Soviet Union!!! Pamoja na KGB yao ule Muungano uko wapi? Vipi kuhusu lile bunge lao imara Duma?Tanzania Kuna watu wasiojulikana ambao wanailinda Katiba hii dhidi ya mtu yeyote hata awe nani atakaeivunja au mwenye mwelekeo wa kuivunja, Watakukalisha chini tu utake usitake. Kumbuka kuwa hata Rais wa Katiba pia analindwa kama inavyolindwa Katiba na Jamhuri. Hata CDF, jaji Mkuu na spika nao wanalindwa kama wengine tu, ni mfumo wa kuilinda Katiba na mipaka ya nchi dhidi ya adui wa ndani na nje.
Yeyote anaetaka serikali 3 atumie njia za wazi za kupata serikali 3, aje na hoja nzito kwanini mfumo uliodumu kwa zaidi ya miaka 60 haufai la sivyo atakuwa anamchezea chatu. Walijaribu wengi lakini hawakufua dafu kwa viwango tofauti. Watu waliojaribu kuutikisa muungano na Katiba ni kama vile akina Sheikh Mzee Abeid Karume, Aboud Jumbe, G55, Sharif Maalim, JPM, Tundu Lissu, salmin armour, nk, wote Hawa walishindwa.
Huwa nashidwa kuwaelewa! Munadai serkali tatu wanashindwa, lkn munashinda mtandaoni mukidai Wazanzibari wasitawale! Sasa mutawazauiaje Wazanzibari kutawala wakati hakuna serikali tatu? Ndo maana huwa nasema tatizo sio muundo wa muungano ila ni ubaguzi tu wa kiimani na wa kimajimbo.Yeyote anaetaka serikali 3 atumie njia za wazi za kupata serikali 3, aje na hoja nzito kwanini mfumo uliodumu kwa zaidi ya miaka 60 haufai la sivyo atakuwa anamchezea chatu. Walijaribu wengi lakini hawakufua dafu kwa viwango tofauti. Watu waliojaribu kuutikisa muungano na Katiba ni kama vile akina Sheikh Mzee Abeid Karume, Aboud Jumbe, G55, Sharif Maalim, JPM, Tundu Lissu, salmin armour, nk, wote Hawa walishindwa.
Waliovunja muungano wa Soviet hawakuwa wasoviet wenyewe, bali wasoviet waliotumiwa na Magharibi. Ndiyo maana sisi tuko macho na kauli za "the world is watching". Which world, who is the world?. Afrika imekufa miungano mingi sana, ukabaki huu tu. Usidhani kuwa na huu wetu haujajaribiwa; lakini kila aliyeujaribu alituachia muungano wetu. Tumeshajua Muungano huu una manufaa mengi kuliko hasara. Hebu ona muungano ulivyotupatia watu hodari kwa kufikiria nje ya box. Bila muungano tungekuwa na viongozi wanaochoma vifaranga vya kuku tu, wapenda vita, makatili, na wanaotaka sifa binafsi hata kama wananchi wanateseka.Kwamba huu Muungano ni imara kuliko Soviet Union!!! Pamoja na KGB yao ule Muungano uko wapi? Vipi kuhusu lile bunge lao imara Duma?
Kwani Wazanzibar wakitawala kuna shida gani? Watanganyika ni wezi kupindukia. skendo zoto za Richmond, Escrow, Melemeta, IPTL, kuuza mashirika na nyumba za serikali, Lissu kupigwa risasi nyingi, kuchoma vifaranga, biashara na majirani kukwama zilitokea wakati watanganyika ndio viongozi. Hebu ona jinsi Mzee Mwinyi (mzanzibar) alivyolivusha taifa kutoka kuvaa mifuko ya safleti hadi kwenda kuvaa suruali na mkanda. Mama Samia amelivusha Taifa kutoka kuchoma vifaranga, watumishi kukosa mishahara na kupanda madaraja, kuvukuza watu barabarani hadi kwenda kwenye kutumia dialogue kutatua migogoro, kulipa kodi kwa heshima, kulipa watu stahiki zao, kuteleza miradi bila mbwembwe nyiiiiingiii.Huwa nashidwa kuwaelewa! Munadai serkali tatu wanashindwa, lkn munashinda mtandaoni mukidai Wazanzibari wasitawale! Sasa mutawazauiaje Wazanzibari kutawala wakati hakuna serikali tatu? Ndo maana huwa nasema tatizo sio muundo wa muungano ila ni ubaguzi tu wa kiimani na wa kimajimbo.
Tambueni kuwa bila mabadiliko ya muundo wa muungano kuwa wa serikali tatu, Wazanzibari wataendelea kutawala halafu mutakuja humu kulalamika. Uamuzi ni wenu, kusuka au kunyoa.
Muungano wa haki na kweli ni wa serikali moja. Hata hata Nyerere alikuwa anaelekea huko polepole, na hata sasa tunaelekea huko polepole. Hiyo ni ajenda ya kudumu, hakuna mtu ataenda kinyume na move hiyo akasalia salama. Hivi vyote unavyoviona sasa hivi ni vituo tu kwenye safari ya kuelekea hukoooo kwenye serikali moja tu aliyoianzisha Mwl Nyerere. Usifikiri Mwl Nyerere alikuwa mpumbavu kuifuta Tanganyika kwa mikono yake mwenyewe. 02 iko karibu zaidi na 01 kuliko 03.Muungano wa serikali tatu ndio WA haki.
Unajidanganya sana ww huwajui vizur wazanzibar 😀Muungano wa haki na kweli ni wa serikali moja. Hata hata Nyerere alikuwa anaelekea huko polepole, na hata sasa tunaelekea huko polepole. Hiyo ni ajenda ya kudumu, hakuna mtu ataenda kinyume na move hiyo akasalia salama. Hivi vyote unavyoviona sasa hivi ni vituo tu kwenye safari ya kuelekea hukoooo kwenye serikali moja tu aliyoianzisha Mwl Nyerere. Usifikiri Mwl Nyerere alikuwa mpumbavu kuifuta Tanganyika kwa mikono yake mwenyewe. 02 iko karibu zaidi na 01 kuliko 03.
Asikwambie mtu wazanzibar wasiopenda Muungano sasa hivi wamebakia wachache sana; ni wale ambao hawajaonja manufaa binafsi ya muungano. Kuna watoto ambao wako pale Shaurimoya Ilala wanauza spea za magari hawataki kusikia habari za kuvunjika muungano.
Kakaa watu hao wanazidi kupungua siku hadi siku. Kizazi kikibakia kile cha 1980s uchungu huo wa wahadhina utapotea wenyewe polepole. Ukishazoea kuishi bara huwezi kutamani kuishi bara any more.Uajidanganya sana ww huwajui vizur wazanzibar 😀
kwamba ufute serikali yao ya mapinduzi ubaki na serikali 1 ya muungano?
Ukitaka kujua wazanzibar wana uzalendo kias gan na nchi yao ni pale maslahi ya Zanzibar yanapojaribiwa na watanganyika
huondoa tofaut zao za itikadi za kisiasa na hungana na kuwa wamoja kuitetea Zanzibar yao
Hawa Watanganyika hawayaoni haya. Wao kwao ni ubaguzi dhidi ya Wazanzivari tu.Kwani Wazanzibar wakitawala kuna shida gani? Watanganyika ni wezi kupindukia. skendo zoto za Richmond, Escrow, Melemeta, IPTL, kuuza mashirika na nyumba za serikali, Lissu kupigwa risasi nyingi, kuchoma vifaranga, biashara na majirani kukwama zilitokea wakati watanganyika ndio viongozi. Hebu ona jinsi Mzee Mwinyi (mzanzibar) alivyolivusha taifa kutoka kuvaa mifuko ya safleti hadi kwenda kuvaa suruali na mkanda. Mama Samia amelivusha Taifa kutoka kuchoma vifaranga, watumishi kukosa mishahara na kupanda madaraja, kuvukuza watu barabarani hadi kwenda kwenye kutumia dialogue kutatua migogoro, kulipa kodi kwa heshima, kulipa watu stahiki zao, kuteleza miradi bila mbwembwe nyiiiiingiii.