ACT Wazalendo: Bajeti ya Serikali 2024/25 ni ya Matajiri na Kulipa Madeni

Wiston Mogha

Senior Member
Joined
Feb 13, 2014
Posts
168
Reaction score
141
NI LEO

Uchambuzi Bajeti Kuu ya Serikali utakaofanywa na ACT Wazalendo utarushwa moja kwa moja na Online Tv mbalimbali. Kuzifahamu tazama katika bango.

Hakikisha Hupitwi!

======

26821527-f646-4a30-9c72-c27394f2676d.jpeg

View: https://www.youtube.com/live/b83BKum1V0w?si=HuB4gP2CaV4cX3hT

"Sote tunafahamu kwamba Juni 13 mwaka huu (2024) serikali iliwasilisha Bungeni bajeti yake ya mwaka 2024/25 ambapo bajeti hii ni ya nne (4) kusomwa tangu Rais Samia Suluhu Hassan aingie madarakani na Waziri wa Fedha ndugu Mwigulu Nchemba, matarajio yetu na matarajio ya Watanzania ilikuwa sera za bajeti ya mwaka huu (2024) zingeweza kugusa maisha ya Watanzania kama ambavyo tumeona katika kipindi cha miaka miwili (2) iliyopita hali za maisha ya Watanzania zimekuwa ngumu na kumękuwa na mijadala mikubwa kuhusiana na tozo zilizoko nchini kwenye maeneo mbalimbali na changamoto tangu tulipomaliza kipindi cha COVID-19, na yale yaliyotokea katika ile miaka na kutetereka kwa uchumi, hali za maisha zilikuwa ni ngumu, bidhaa zilikuwa zimepanda bei sana na kwa hiyo maisha ya Watanzania yalikuwa yakielezwa kwa ugumu mkubwa" -Mchinjita"

Kwa hiyo tulitegemea serikali imeshajipanga vyakutosha kuja kukabili hizo changamoto, kwa hiyo mapendekezo ya bajeti ya mwaka huu (2024) ukiangalia kwa ujumla wake kwa kweli yanakuja kushughulikia masuala ya utawala na kulipa madeni kitu ambacho tumekuwa tukioneshwa kama ni sehemu ya udhaifu mkubwa wa namna ambavyo tunaendesha uchumi wetu kwa sasa, inaonekana serikali inatekeleza sera za kuwanufaisha wafanyabiashara wakubwa kwa matarajio kuwa fedha hizi zitarudi kwa wananchi kutokea kwa wafanyabiashara, sera za uchumi za namna hii haziwezi kamwe kuwaondoa Watanzania kwenye dimbwi la umasikini, sera zinazofaa ni zile za kuwawezesha wananchi ambapo sisi ACT Wazalendo tunaziita 'Taifa la wote, maslahi ya wote" -Mchinjita

Pia soma: Waziri Mwigulu awasilisha Bajeti Kuu ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025

Makamu Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Tanzania Bara Isihaka Mchinjita amezungumza hayo leo, Jumamosi Juni 22.2024 wakati chama hicho kilipokutana na wanahabari kwa ajili ya kuchambua mapendekezo ya bajeti kuu ya serikali iliyowasilishwa Bungeni hivi karibuni.

"Katika bajeti (kuu ya serikali) ya mwaka 2023/24 serikali ilitarajia kukusanya jumla ya shilingi trilioni 44.39 kutoka katika vyanzo vya ndani na nje hadi Aprili 2024 jumla ya shilingi trilioni 35.25 zilikusanywa kutoka vyanzo hivyo, makusanyo haya ni sawa na aslimia 79.4 ya malengo yaliyowekwa na serikali ili kutekeleza vipaumbele vyake.

Mwenendo huu wa ukasanyaji wa mapato ni wazi kuwa malengo iliyojiwekea hayatofikiwa, upungufu wa shilingi trilioni 9.14 ambapo muda uliobakia kukamilisha mwaka huu wa fedha ni miezi miwili pekee, kwa hiyo serikali inapaswa ikusanye kwa wastani wa trilioni 4.57 kwa kila mwezi jambo ambalo halitoweza kufikiwa kwa kuwa wastani wa miezi kumi iliyopita ni kukusanya trilioni 3.5 kwa mwezi, ni wazi kuwa upungufu wa malengo ya ukusanyaji wa mapato utaenda kuathiri uwezo wa serikali kukamilisha vipaumbele, na kwa sehemu kubwa maeneo yatakayo athiriwa zaidi ni kwenye utekelezaji wa miradi ya maendeleo"

Kwa miaka mitatu mfululizo mwenendo wa makusanyo umekuwa chini ya makadirio na malengo yaliyowekwa, sababu zilizosababisha kutokufikiwa kwa malengo ya makusanyo ya mwaka wa fedha wa 2023/24, rushwa na uzembe unaosababisha kushindwa kukusanya mapato ya serikali kama ilivyoelezwa katika ripoti ya CAG, (upotevu kwenye POS/ kutofanya malipo kwa control namba) utoroshwaji mkubwa wa madini nchini, kwa mfano kwa mara moja tu madini ya bilioni 3.7 yaliamatwa yakiwa yanatoroshwa, hii ina maana kuwa eneo hili kuna upotevu mkubwa wa mapato.

Utegemezi wa mikopo na misaada, serikali inashindwa kutanua wigo wa vyanzo vya mapato ambavyo havitaumiza wananchi badala yake inawakamua na kuwabebesha mzigo mkubwa wananchi walewale, mfano mama ntilie, wafanyabiashara wadogo ndio wamekua wakibanwa na kupata usumbufu mkubwa kutoka kwa TRA kiasi cha kufikia kufunga biashara zao, kwa hali hii mapato ya serikali hayatafikiwa ila mifuko ya watu wachache itaendelea kutuna"

Waziri Mkuu Kivuli wa ACT Wazalendo ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Tanzania Bara Isihaka Mchinjita amezungumza hayo leo, Jumamosi Juni 22.2024 wakati chama hicho kilipokutana na wanahabari kwa ajili ya kuchambua mapendekezo ya bajeti kuu ya serikali iliyowasilishwa Bungeni hivi karibuni.
 
NI LEO

Uchambuzi Bajeti Kuu ya Serikali utakaofanywa na @ACTwazalendo utarushwa moja kwa moja na Online Tv mbalimbali. Kuzifahamu tazama katika bango.

Hakikisha Hupitwi!

@ACTBarazaKivuli
#TaifaLaWote #MaslahiYaWote
Asante kwa taarifa, hii sio ya kukosa.
P
 
Safi sana ACT wazalendo kwa kuonesha tofauti yenu na ccm ktk mtazamo wa masuala na siyo matukio.

Japo mwaka huu sijaona mkitusomea bajeti yenu mbadala.
 
Hawa ACT walikuwa na baraza la mawaziri kimvuli
Lkn ktk mapendekezo na mipangao mbadala wapo kmya
 
NI LEO

Uchambuzi Bajeti Kuu ya Serikali utakaofanywa na @ACTwazalendo utarushwa moja kwa moja na Online Tv mbalimbali. Kuzifahamu tazama katika bango.

Hakikisha Hupitwi!

@ACTBarazaKivuli
#TaifaLaWote #MaslahiYaWote

View attachment 3022770
Safi Sana nitaangalia hongera mko vizuri sio kama Akina Lisu bajeti inaendelea hachangii bajeti anaonngelea Tu mambo ya Abdul na mama Yake na wasichana WA Singida wanaojiuza Dar es salaam

Hongereni ACT wazalendo kujikiya kwenye issue ya kitaifa serious bajeti nitawasikiliza
 
Hawa ACT walikuwa na baraza la mawaziri kimvuli
Lkn ktk mapendekezo na mipangao mbadala wapo kmya
Basi washauriwe , waandaye bajeti mbadala. Binafsi nawaelewa sana hawa jamaa.
 
1719050906158.png

"Sote tunafahamu kwamba Juni 13 mwaka huu (2024) serikali iliwasilisha Bungeni bajeti yake ya mwaka 2024/25 ambapo bajeti hii ni ya nne (4) kusomwa tangu Rais Samia Suluhu Hassan aingie madarakani na Waziri wa Fedha ndugu Mwigulu Nchemba, matarajio yetu na matarajio ya Watanzania ilikuwa sera za bajeti ya mwaka huu (2024) zingeweza kugusa maisha ya Watanzania kama ambavyo tumeona katika kipindi cha miaka miwili (2) iliyopita hali za maisha ya Watanzania zimekuwa ngumu na kumękuwa na mijadala mikubwa kuhusiana na tozo zilizoko nchini kwenye maeneo mbalimbali na changamoto tangu tulipomaliza kipindi cha COVID-19, na yale yaliyotokea katika ile miaka na kutetereka kwa uchumi, hali za maisha zilikuwa ni ngumu, bidhaa zilikuwa zimepanda bei sana na kwa hiyo maisha ya Watanzania yalikuwa yakielezwa kwa ugumu mkubwa" -Mchinjita"

Kwa hiyo tulitegemea serikali imeshajipanga vyakutosha kuja kukabili hizo changamoto, kwa hiyo mapendekezo ya bajeti ya mwaka huu (2024) ukiangalia kwa ujumla wake kwa kweli yanakuja kushughulikia masuala ya utawala na kulipa madeni kitu ambacho tumekuwa tukioneshwa kama ni sehemu ya udhaifu mkubwa wa namna ambavyo tunaendesha uchumi wetu kwa sasa, inaonekana serikali inatekeleza sera za kuwanufaisha wafanyabiashara wakubwa kwa matarajio kuwa fedha hizi zitarudi kwa wananchi kutokea kwa wafanyabiashara, sera za uchumi za namna hii haziwezi kamwe kuwaondoa Watanzania kwenye dimbwi la umasikini, sera zinazofaa ni zile za kuwawezesha wananchi ambapo sisi ACT Wazalendo tunaziita 'Taifa la wote, maslahi ya wote" -Mchinjita

Makamu Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Tanzania Bara Isihaka Mchinjita amezungumza hayo leo, Jumamosi Juni 22.2024 wakati chama hicho kilipokutana na wanahabari kwa ajili ya kuchambua mapendekezo ya bajeti kuu ya serikali iliyowasilishwa Bungeni hivi karibuni.

"Katika bajeti (kuu ya serikali) ya mwaka 2023/24 serikali ilitarajia kukusanya jumla ya shilingi trilioni 44.39 kutoka katika vyanzo vya ndani na nje hadi Aprili 2024 jumla ya shilingi trilioni 35.25 zilikusanywa kutoka vyanzo hivyo, makusanyo haya ni sawa na aslimia 79.4 ya malengo yaliyowekwa na serikali ili kutekeleza vipaumbele vyake.

Mwenendo huu wa ukasanyaji wa mapato ni wazi kuwa malengo iliyojiwekea hayatofikiwa, upungufu wa shilingi trilioni 9.14 ambapo muda uliobakia kukamilisha mwaka huu wa fedha ni miezi miwili pekee, kwa hiyo serikali inapaswa ikusanye kwa wastani wa trilioni 4.57 kwa kila mwezi jambo ambalo halitoweza kufikiwa kwa kuwa wastani wa miezi kumi iliyopita ni kukusanya trilioni 3.5 kwa mwezi, ni wazi kuwa upungufu wa malengo ya ukusanyaji wa mapato utaenda kuathiri uwezo wa serikali kukamilisha vipaumbele, na kwa sehemu kubwa maeneo yatakayo athiriwa zaidi ni kwenye utekelezaji wa miradi ya maendeleo"

Kwa miaka mitatu mfululizo mwenendo wa makusanyo umekuwa chini ya makadirio na malengo yaliyowekwa, sababu zilizosababisha kutokufikiwa kwa malengo ya makusanyo ya mwaka wa fedha wa 2023/24, rushwa na uzembe unaosababisha kushindwa kukusanya mapato ya serikali kama ilivyoelezwa katika ripoti ya CAG, (upotevu kwenye POS/ kutofanya malipo kwa control namba) utoroshwaji mkubwa wa madini nchini, kwa mfano kwa mara moja tu madini ya bilioni 3.7 yaliamatwa yakiwa yanatoroshwa, hii ina maana kuwa eneo hili kuna upotevu mkubwa wa mapato.

Utegemezi wa mikopo na misaada, serikali inashindwa kutanua wigo wa vyanzo vya mapato ambavyo havitaumiza wananchi badala yake inawakamua na kuwabebesha mzigo mkubwa wananchi walewale, mfano mama ntilie, wafanyabiashara wadogo ndio wamekua wakibanwa na kupata usumbufu mkubwa kutoka kwa TRA kiasi cha kufikia kufunga biashara zao, kwa hali hii mapato ya serikali hayatafikiwa ila mifuko ya watu wachache itaendelea kutuna"

Waziri Mkuu Kivuli wa ACT Wazalendo ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Tanzania Bara Isihaka Mchinjita amezungumza hayo leo, Jumamosi Juni 22.2024 wakati chama hicho kilipokutana na wanahabari kwa ajili ya kuchambua mapendekezo ya bajeti kuu ya serikali iliyowasilishwa Bungeni hivi karibuni.
https://x.com/Jambotv_/status/1804456914002002118/photo/1
 
Dawa ya Deni Kulipa

Africa kusini wamemrudisha Kaburu serikalini kupitia mlango wa Nyuma 🐼
 
Serikali ikiwa na madeni mnalalamika, ikiwa inalipa madeni mnalalamika, kuwa upinzani ndio kukataa kila kitu au kukubaliana na vilivyosawa na kutoa ushauri wa nini kifanyike kwa kile ambacho mwaona hakipo sawa?!, kwa COVID mbona walisema tulioyumba sio sisi wananchi tu bali hata serikali iliyumba, na serikali duniani vitu viliyumba, anyway waziri mkuu kivuli pambaneni mshike hatamu pia ili tuone na nyie mtaongozaje au mtasema hamkuwepo wakati huo ndio mwapambana kulipa madeni.
 
Back
Top Bottom