LGE2024 ACT Wazalendo: CCM na Wasimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa waache kuwatisha na kuwashawishi wagombea wa upinzani kujiondoa kwenye uchaguzi

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2012
Posts
6,067
Reaction score
10,938
Kamati ya Uongozi Taifa ya ACT Wazalendo imekutana kwenye kikao chake cha kawaida kilichofanyika jana tarehe 02 Novemba, 2024 katika Ukumbi wa Jurna Duni Haji, Makao Makuu ya ACT Wazalendo, Dar es salaam chini ya uenyekiti wa Kiongozi wa Chama Ndugu Dorothy Semu.

Pamoja na mambo mengine, Kamati ya Uongozi imepokea taarifa ya maandalizi ya Chama kushiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji, na mwenendo wa uchaguzi huo na kuifanyia tathmini na tafakuri ya kina na kutoa maelekezo mbalimbali kwa vyombo na ngazi mbalimbali za Chama.

1. Kamati ya Uongozi ya Chama Taifa inawapongeza viongozi wote wa Chama wa ngazi zote kwa ushiriki wao katika mchakato wa uchaguzi na kuhakikisha Chama kinaweka wagombea katika kila ngazi inayogombewa. Aidha, Kamati ya Uongozi imefurahishwa na mwamko wa wanachama wa ACT Wazalendo katika uchaguzi kwa kujitokeza kwa wingi kuchukua na kurejesha fomu za kugombea nafasi mbalimbali. Kwa mujibu wa takwimu za wagombea zilizokusanywa mpaka sasa kutoka sehemu mbalimbali za nchi, ACT Wazalendo kimedhihirisha ukuaji wake na uimara wake kama Chama cha kitaifa.

2. Hata hivyo, Kamati ya Uongozi Taifa imesikitishwa na mwenendo usioridhisha wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa hasa kwenye maeneo yafuatayo;-

1) Hujuma, ubabaishaji na udanganyifu kwenye zoezi la uandikishaji wapigakura uliolenga kukipendelea Chama cha Mapinduzi. Mathalani udanganyifu wa idadi ya wapigakura walioandikishwa kuwa ni 31,282,331 huku mwitikio halisi wa kujiandikisha vituoni ukionesha kuwa ni hafifu.

ii)Changamoto kwenye zoezi la uchukuaji na urejeshwaji wa fomu ikiwemo baadhi ya wasimamizi kufunga ofisi (mfano Kondoa Vijijini, Newala, Tunduma, Ulyankulu n.k), kukataa kupokea fomu za wagombea na kukataa maelekezo ya Waziri wa TAMISEMI ya kuvipa vyama uhuru wa kuchagua ngazi ya chini ya kudhamini wagombea (mfano, Kijiji cha Wari Ndoo Kata ya Machame Kaskazini Hai, na maeneo mbalimbali jimbo la Ruangwa).

ⅲ) Chama cha Mapinduzi na baadhi ya Wasimamizi wa Uchaguzi kuwapigia simu wagombea waliorejesha fomu kuwatisha na kuwashawishi wajitoe kuwa wagombea (mfano, Kijiji cha Miuta, Tandahimba na Mtaa wa Kanenwa Kata ya Kishiri, Nyamagana Mwanza)

Kamati ya Uongozi Taifa imetoa maelekezo yafuatayo;-

1. Ofisi ya Katibu Mkuu imeelekezwa kumwandikia Msimamizi wa Uchaguzi orodha ya wagombea wote wa ACT Wazalendo walioshindwa kuchukua na kurejesha fomu kwa sababu ya Wasimamizi wa Uchaguzi kutofungua Ofisi ili wagombea husika warejeshwe kwenye orodha ya wagombea.

2. Ofisi ya Katibu Mkuu kuwasiliana na vyama vingine makini vya siasa na wadau wengine wa demokrasia nchini ili kuandaa kampeni kubwa ya kitaifa ya kuhamasisha umma kupiga kura ya HAPANA kwa wagombea wote wa CCM ambao wamebaki peke yao.

3. Chama kiendelee na mpango kabambe wa kampeni na kulinda kura kwenye maeneo yote ambayo ACT Wazalendo kina wagombea ili kuwapa nafasi wananchi kupata uwakilishi bora katika vijiji, mitaa na vitongoji vyao.

4. Ilani ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ya ACT Wazalendo izinduliwe wiki moja kabla ya tarehe ya kampeni kuanza.

WITO WA KAMATI YA UONGOZI KWA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
Kamati ya Uongozi Taifa ya ACT Wazalendo inamkumbusha Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa uchaguzi wa Serikali za Mitaa utatumika kupima iwapo ana nia ya dhati ya kujenga misingi imara ya kidemokrasia nchini kupitia falsafa yake ya 4R au ameamua kuizika rasmi misingi ya kidemokrasia na kuirejesha nchi kwenye njia ya udikteta wa mtangulizi wake. Chaguo lipo mikononi mwake na wakati sahihi wa kuamua ni sasa!

Tunatoa wito kwa Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;

1. Kuzuia mara moja vitendo vya makada wa CCM na wasimamizi wa uchaguzi kuwatisha na kuwashawishi wagombea wa upinzani kujiondoa kuwa wagombea.

2. Ahakikishe zoezi la uteuzi wa wagombea linaendeshwa kwa haki.

3. Ahakikishe hatua zilizosalia katika mchakato wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa hasa hatua za uapishwaji wa mawakala, upigaji kura, kuhesabu kura na utangazaji wa matokeo zinazingatia misingi ya haki kwa mujibu wa Sheria na Kanuni zinazoongoza uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

A1.jpg
A2.jpg
 
Na nyie mkipata ruzuku mnatumia kula raha ubeligiji, chama hakina hata senti
 
CCM B inatembea na codes za chadema
 
View attachment 3142600View attachment 3142601
Gentleman,
kwani chadema ina wagombea Serikali za mitaa na vijiji?

mbona kata yangu yenye vijiji vi5 haina mgombea wa upinzani hata moja ispokua kitongoji kimoja tu na kuna mgombea wa upinzani dhaifu zaidi asie wa Chadema?🐒
 
Kaka wagombea wa vyama pinzani wanatishwa, wanatekwa, wanauawa n.k inajenga hofu na wasiwasi wa kuendelea kujitangaza kwa wapinzani (chama tawala) lakini naimani tutafika tu !.
 
sasa kiongozi anatishwa na anatishika, anafaa kweli huyo gentleman?

sasa atamuongoza nani kama kiongozi huyo ana hofu? Halafu, wanauawa wapi hao wapinzani?
kata yangu ya vijiji v5, mbona kiongozi mpinzani kwenye kitongoji hana hofu?

huenda wanauana huko kwenye chaguzi za ndani kwenye vyama vyao 🐒
 
Back
Top Bottom