Pre GE2025 ACT Wazalendo: CCM siyo chama cha siasa tena. Zamani ilikuwa inatumia dola ili kuiba uchaguzi, sasa Dola inaitumia CCM kuiba uchaguzi

Pre GE2025 ACT Wazalendo: CCM siyo chama cha siasa tena. Zamani ilikuwa inatumia dola ili kuiba uchaguzi, sasa Dola inaitumia CCM kuiba uchaguzi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

mwanamwana

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
1,309
Reaction score
4,798
Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, ndugu Ado Shaibu amejibu kauli ya Ally Hapi kuwa Dola iwashughulikie wanaotaka kuzuia uchaguzi, ambapo amesema kuwa CCM siyo chama cha siasa tena, kwasababu sifa ya chama cha siasa ni lazima kiwe na uwezo wa kuleta ushindani.

CCM hii ya sasa siyo ile tuliyokuwa tunaijua zamani, ambayo kwenye baadhi ya maeneo kweli ulikuwa unashindana nayo. Kuna maeneo CCM ni dhaifu sana, na kuna maeneo unaona kabisa unashindana nayo, ile CCM haipo kwa mujibu wa Halmashauri kuu.

Kupata taarifa na matukio ya kimkoa kuhusu Uchaguzi Serikali za Mitaa ingia hapa: LGE2024 - Special Thread: Orodha ya Mijadala ya Mikoa yote Tanzania Bara inayoshiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Sasa hatupambani na CCM, tunapambana na dola. Utofauti wa zamani na wa sasa ni kwamba zamani CCM ilikuwa inatumia dola ili kuweza kuiba uchaguzi. Hali ya sasa ni Dola inaitumia CCM kuiba uchaguzi.

CCM wenyewe kwenye baadhi ya maeneo hawajui uchaguzi uliibwaje, wanaweza wakajua kulikuwa kuna hili na lile, na uchaguzi wa leo huwezi ukasikia eti uchaguzi unashangiliwa. Dola inaipa CCM asilimia hadi wenyewe wanahangaa, wenyewe hawajui.

Kwa hiyo Ally Hapi akisema dola iwashughulikie, sisi tayari tunajua adui yetu tunayepambana naye, atakayekuwa anapanga kutushughulikia, na sisi tunajipanga kukabiliana naye ni Dola.

Pia soma > LGE2024 - ACT Wazalendo: Vyombo vya Dola vilitumika kuweka kura bandia kwenye maboksi ya kura

 
Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo ACT Wazalendo, Ado Shaibu Ado Shaibu, akijibu kauli ya Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi CCM, Ally Hapi aliyosema vyombo vya Dola vishughulike na watakaojaribu kuvuruga uchaguzi.

"Tulijiuliza CCM kama Chama cha cha siasa kipo? Tukafikia hitimisho kuwa CCM siyo chama cha siasa kwa sababu sifa ya chama cha siasa ni lazima kiwe na uwezo wa kuleta ushindani. CCM hii ya siasa siyo ile tuliyokuwa tunaijua zamani

CCM zamani ilikuwa inatumia dola ili kuiba uchaguzi, hali ya sasa haipo hivyoo, hali ya sasa ni dola inaitumia CCM kuiba uchaguzi" - Ado Shaibu

Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa:
Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
 

Attachments

  • 5811771-84b12f6d5ff81d807821a183416ac2ed.mp4
    648.4 KB
Chama ndiyo kinaunda Dola....Chama ndiyo kinachagua nani aongoze dola...Kwahiyo ukipambana na Chama unapambana na dola.

Unavyokosoa haukosoi mwenyekiti wa chama bali unakosoa rais aliyepewa kijiti na chama...haukosoi mambo ya chama bali unakosoa mambo ya dola.

kama unapambana na chama basi kosoa mambo yao ya chama tu hapo ndiyo utaeleweka.
 
Back
Top Bottom