Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, ndugu Ado Shaibu amejibu kauli ya Ally Hapi kuwa Dola iwashughulikie wanaotaka kuzuia uchaguzi, ambapo amesema kuwa CCM siyo chama cha siasa tena, kwasababu sifa ya chama cha siasa ni lazima kiwe na uwezo wa kuleta ushindani.
CCM hii ya sasa siyo ile tuliyokuwa tunaijua zamani, ambayo kwenye baadhi ya maeneo kweli ulikuwa unashindana nayo. Kuna maeneo CCM ni dhaifu sana, na kuna maeneo unaona kabisa unashindana nayo, ile CCM haipo kwa mujibu wa Halmashauri kuu.
Sasa hatupambani na CCM, tunapambana na dola. Utofauti wa zamani na wa sasa ni kwamba zamani CCM ilikuwa inatumia dola ili kuweza kuiba uchaguzi. Hali ya sasa ni Dola inaitumia CCM kuiba uchaguzi.
CCM wenyewe kwenye baadhi ya maeneo hawajui uchaguzi uliibwaje, wanaweza wakajua kulikuwa kuna hili na lile, na uchaguzi wa leo huwezi ukasikia eti uchaguzi unashangiliwa. Dola inaipa CCM asilimia hadi wenyewe wanahangaa, wenyewe hawajui.
Kwa hiyo Ally Hapi akisema dola iwashughulikie, sisi tayari tunajua adui yetu tunayepambana naye, atakayekuwa anapanga kutushughulikia, na sisi tunajipanga kukabiliana naye ni Dola.
Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo ACT Wazalendo, Ado Shaibu Ado Shaibu, akijibu kauli ya Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi CCM, Ally Hapi aliyosema vyombo vya Dola vishughulike na watakaojaribu kuvuruga uchaguzi.
Your browser is not able to display this video.
"Tulijiuliza CCM kama Chama cha cha siasa kipo? Tukafikia hitimisho kuwa CCM siyo chama cha siasa kwa sababu sifa ya chama cha siasa ni lazima kiwe na uwezo wa kuleta ushindani. CCM hii ya siasa siyo ile tuliyokuwa tunaijua zamani
Ukweli mchungu Sana ni kwamba Wapinzani wa Siasa nchini Tanzania wanapambana na Dola hususani Tiss na Polisi. Hawapambani na CCM.
Huu ni Ukweli mchungu.
Ukweli mchungu Sana ni kwamba Wapinzani wa Siasa nchini Tanzania wanapambana na Dola hususani Tiss na Polisi. Hawapambani na CCM.
Huu ni Ukweli mchungu.