Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Chama cha ACT Wazalendo kinatoa tamko muda huu kuhusu kutekwa kwa Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana, Abdul Nondo, nakutelekezwa usiku wa kuamkia leo katika fukwe za Coco Beach, Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa taarifa ya Jeshi la Polisi, Nondo alisaidiwa na dereva wa bodaboda aliyemfikisha katika ofisi za ACT Wazalendo.
Kwa niaba ya Uongozi wote wa Ngome ya Vijana, ACT Wazalendo tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa Uongozi wetu wa Chama kwa kusimama na kupambana nasi kwa zaidi ya saa 18 tangu tukio la kutekwa na Maafisa wa Jeshi la Polisi mpaka kupatikana kwa kiongozi wetu wa Ngome ya Vijana Abdul Nondo.
Viongozi wetu kwa namna walivyoshughulika nasi katika kadhia hii wametupa nguvu kubwa vijana kwamba hakuna litakalotukuta lolote bila msaada wao, mshikamano wao, ufuatiliaji wao, mwongozo wao, na ujasili wao umekuwa darasa kubwa kwetu na tunajivunia kuwa vijana wa ACT Wazalendo na tunajivunia kuwa Wanachama wa Chama chetu.
Pamoja na viongozi wetu ambao pia ndio walezi wetu Kisiasa tunachukua fursa hii kumshukuru kwa dhadhi Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, John Mnyika kwa ushirikiano wake wa kututaarifu kwa haraka kuhusu tukio hili punde tu alipo pokea taarifa kutoka kwaa msamaria mwema wa Stendi ya Magufuli.
Tunashukuru pia Wananchi waliokuwepo Stendi ya Magufuli kwa kutoa taarifa za awali na Watanzania kwa ujumla pasipo kujali itikadi za ksiasa, tumeshikamana tena kupinga ushamba wa utekaji na kusimama na kusema kwa pamoja kwa ajili ya haki.
Ngome ya vijana hatuna sababu yoyote mpaka sasa ya kulishukuru Jeshi la Polisi kutokana na tukio zima lililotokea, tunasikitishwa sana na Jeshi la Polisi kwakua tunaona halichukui suala la watu kutekwa na kupotezwa kwa umakini wa aina yoyote kiasi tumebaki na maswali mengi kuhusu tukio zima la utekwaji kwa Mwenyekiti wetu ila kikubwa walichofanya ni kutoa matamko ya jumla jumla.
Pia soma: