ACT Wazalendo wakiambiwa ni ccm b wasiwe wabishi na kubaki kusemasema wanasingiziwa kuwa ni pro ccm. Wakubali au wakatae habari ndiyo hiyo na wanaimba na kucheza midundo ya ccm. Wale si wapinzani bali ni washirika wa CCM katika serikali. Ni wamoja na hawawezi kupingana. Cdm ndiyo chama cha upinzani japo safari hii kina woga mkubwa wa kujenga hoja.
ACT hakiwezi kuwa tripple standard, kwa maana kwamba ni ngumu kuwa na ushirikiano na ccm kwa upande mmoja na upande mwingine kiwe na ushirikiano na cdm, katikati kibaki chenyewe kama chama cha upinzani. Labda kiwe chama cha upinzani kwa cdm. Kwa hali ilivyo sasa ukija uchaguzi mkuu act itaathiri kura za upinzani na kusababisha ccm ipate ushindi mnono. Huu ni mtazamo hafifu wenye ukweli mtupu na halisi.