Pre GE2025 ACT-Wazalendo jengeni upinzani wa kweli. Mlitaka Tume Huru ya Uchaguzi leo mmeshindwa kuipigania

Pre GE2025 ACT-Wazalendo jengeni upinzani wa kweli. Mlitaka Tume Huru ya Uchaguzi leo mmeshindwa kuipigania

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Matulanya Mputa

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2023
Posts
245
Reaction score
655
Chama cha ACT-WAZALENDO, tambueni nyie ni chama cha upinzani siyo chama rafiki cha CCM kumbukeni nyie ndiyo kipaumbele chenu kilikuwa tume huru ya uchaguzi muliamini kuwa tume huru ya uchaguzi ikipatikana basi uchaguzi utakuwa wa huru na haki.

Pia kumbukeni Chadema walikwepa mtego wa tume huru ya uchaguzi sababu walitoa hoja zao kuwa huwezi kuwa na tume huru ya uchaguzi wakati tume ya uchaguzi inabebwa na katiba, ndiymana wakataka katiba ibadilishwe au ifanyiwe marekebisho madogo.

CHADEMA waliona mbali kuwa marekebisho madogo ya katiba hasa katika ibara inayohusu tume ya uchaguzi ndyo ingekuwa msingi mzuri wa kupata tume huru ya uchaguzi.

- ACT Wazalendo yataka iundwe Tume Huru ya Uchaguzi na ndiyo Isimamie Uchaguzi wa serikali za Mitaa!

ACT-WAZALENDO hawakutaka katiba bora hawakujua katiba ndyo msingi wa kupata tume huru ya uchaguzi.
Rejea mapingamizi ya mawakili wa serikali kupitia kesi iliyopo mahakama ni, wao hoja yao kuwa ili ufanye marekebisho ya kuifanya TAMISEM isisimae uchaguzi ni kuwa MAHAKAMA HAIWEZI TOA MAAMUZI MPAKA BUNGE LIFANYE MABADILIKO YA KATIBA (wanasheria mtanipa msaada wa kisheria kuweka sawa hizo hoja).

Ni nini tafsiri yake CHADEMA waliona mbali na maamuzi yeyote ambayo yatatolewa na mahakama wasilaumiwe.

Bali ACT-WAZALENDO mumewaingiza au mumeingia mkenge ambao leo mumeshindwa kutoka badala yake mawakili wa CHADEMA, na wanaharakati wanajaribu kuwanasua lakini wakifanikiwa tutawapongeza CHADEMA.
Pia kumbusho ACT-WAZALENDO msiwe kama mumeshika dola, japo mnamikakati mizuri ila kumbukeni CCM hawatakuwa na huruma siku ya uchaguzi,

Napenda kuwasilisha naenda kula mtori kwa shishi food.
 
Zitto sio aina ya watu wa kuaminika hata kidogo. Yeye ni mchungaji wa mshahara, akitangaziwa posho kidogo, na mtazamo wake unabadilika
 
Back
Top Bottom