Leo, tarehe 6 Machi 2025, Wakili Mwanaisha Mndeme amewasilisha shauri la uchaguzi katika Mahakama ya Wilaya ya Mkuranga, Mkoa wa Pwani, akiwawakilisha waliokuwa wagombea wa uchaguzi wa serikali ya kijiji cha Tambani, wilayani Mkuranga, kupitia chama cha ACT Wazalendo.
Shauri hilo limewasilishwa kupinga matokeo na mwenendo wa uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji uliofanyika tarehe 27 Novemba 2024. Kesi hiyo leo imekuja kwa ajili ya kutajwa, huku kusikilizwa rasmi kukitarajiwa kuanza tarehe 12 Machi 2025.
Chama cha ACT-Wazalendo kimefungua mashauri ya uchaguzi 51 ya kupinga matokeo na mwenendo wa uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji uliofanyika Novemba 27, 2024 na kusimamiwa na Ofisi ya Rais-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi). Kesi hizo zimefunguliwa katika mahakama za...