abel p
Member
- May 8, 2020
- 54
- 61
Ndugu zangu kwanza kabisa nimshukuru mwenyezi Mungu kwa wingi wa Rehema zake, Nijikite kwenye mada yangu kama kichwa cha habari kinavyo jieleza ACT-Wazalendo na CHADEMA mnadeni kubwa kwa watanzania.
Ndugu zangu waswahili husema uungwana ni kitendo na ukiahidi tekeleza, itakumbukwa kwenye mkutano mkuu wa ACT-Wazalendo kiongozi mkuu wa ACT-Wazalendo ndugu Zitto aliwaahidi watanzania kuwa wao kama ACT-Wazalendo watahakikisha wanafanya kila liwezekanalo ili upinzani usimamishe mgombea mmoja wa uraisi kati ya Lissu au Membe.
Na kana kwamba hiyo haitoshi kwenye mkutano huo Mhe. Zitto Wazalendo aliwapandisha jukwaani mh Membe na mh Lissu na kuwatambulisha kama wagombea ambao mmoja wapo kati ya wawili hao atapeperusha bendera ya upinzani.
Sasa wakati umewadia tafadhali mh Zitto Kabwe na Mhe. Mbowe wakati ndio huu jitokezeni mbele ya watanzania mtueleze twende na nani kati ya Lissu ua Membe.