Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 15,101
- 56,054
1. Mueleze bila kupepesa macho tatizo la utapiamlo kwa watoto wachanga na mna mikakati gani. Waziri wa Afya ummy Mwalimu amesema takriban asilimia 31.8 ya vitoto vichanga nchini chini ya umri wa miaka 5 vina utapiamlo, na vina hatari ya udumavu wa akili. Hili jambo ni hatari sana maana hawa ni taifa la kesho.
Iwapo tutakuwa na watoto waliodumaa akili, tutakuja kuwa na Taifa la watu wenye IQ ndogo sana na hivyo hatuwezi kuendelea
2. Namna ya kutatua tatizo la ajira
Serikali ya Magufuli imeshindwa kabisa kutengeneza ajira rasmi ambazo ni za maana. Serikali haiajiri ukilinganisha na serikali iliyopita. Vijana wetu wanamaliza shule za sekondari na vyuo vikuu lakini wanasaga lami, ajira hakuna. ACT na CHADEMA lazima muelezee mna majibu gani juu ya suala la ajira
3. Maslahi ya wafanyakazi
Ilani lazima ijibu changamoto ya kutothaminiwa kwa watumishi wa umma kwa maslahi yao kutopewa kipaumbele. Ilani lazima zielezee zintafanya nini juu ya malimbikizo ya wafanyakazi, lazima zielezee kuhusu nyongeza za mishahara za wafanyakazi wa umma ambazo zipo kisheria, vitu ambavyo serikali hii ya awamu ya Tano imevizuia kibabe kinyume cha mikata ya ajira ya watumishi na bila hata majadiliano yoyote na wafanyakazi.
4. Kuhusu wakulima
Lazima ilani zielezee, zina mpango gani makhsusi juu ya kumsaidia mkulima, Lazima ilani ionyeshe kuwa itakuwa ni jukumu la serikali kusaidia kutafuta masoko ya mazao ya kulima kupitia diplomatic missions mbalimbali zilizoko huko nje ya nchi. Si vibaya tukaanzisha balozi za uwekezaji na kilimo huko nje kama mpango mkakati wa diplomasia ya kiuchumi.
Ilani lazima ichukue wazo la Kilimo Kwanza na kuliboresha.
Ilani lazima iseme wazi na kwa sauti kubwa, ina mpango gani juu ya wakulima wa korosho waliofanyiwa dhulma kubwa na utawala huu. Ilani. lazima ieleze mikakati ya kukuza kilimo kwa mazao yote ya chakula na biashara.
5. Kuhusu ufisadi
Ilani lazima zielezee kwa uwazi, na kwa lugha yenye kueleweka namna ufisadi utakavyopigwa vita. Tumeona awamu hii ya Tano ilikuja na gia ya kupambana na ufisadi lakini imefanya usanii wa kutisha kwenye hii vita. Kwa mfano tuliambiwa kuwa Lugola na Andengenye wameingia mkataba wa kifisadi wa shilingi takriban Trillion 1, lakini mpaka leo hii wako uraiani, na Andegenye kapewa cheo cha ukuu wa mkoa. Sasa tunataka ilani ziseme wazi kuwa zina mkakati gani usio wa kisanii juu ya suala hili
6. Kwenye suala la Elimu
Ilani lazima ziseme kuwa zitapunguza makato ya bodi ya mikopo kutoka 15% hii ya sasa kwa mwezi hadi 5% na ipunguze retention fee kutoka 6% hadi 3%. Haya makato yanasababisha maisha ya wananchi kuwa magumu. Na ilani lazima iseme kuwa itaifanyia restructuring bodi ya mikopo iwe more transparent, iache kubambikizia watu madeni ambayo hayapo na kwamba itawekeza kwenye IT ili kufanya kila mdaiwa aweze kutrack vizuri deni lake online na status ya ulipaji wake. Pia Ilani lazima iseme kuwa itafanya elimu hadi ya kidato cha sita kuwa ni bure!.
Kadhalika lazima Ilani iseme kuwa itatoa mikopo kwa wanafunzi wote kwa 100% bila kujali mkondo wa masomo ambayo mwanafunzi anachukua!
7. Ilani lazima izungumzie haja ya kuwapa wananchi katiba mpya
Hii katiba ya sasa imepitwa na wakati, ni katiba iliyoundwa kipindi cha chama kimoja, inaweka mayai yetu yote mikononi mwa mtu mmoja aitwaye rais, tukipata rais asiyeheshimu haki za watu matokeo yake yanakuwa kama haya tuliyoyaona kwenye utawala wa awamu hii, kwamba anaweza kufanya lolote na huwezi kumchukulia hatua za kisheria
8. Ilani lazima ieleze kuhusu kuwalipa fidia wale wote waliovunjiwa nyumba za Kimara-Mbezi, hawa wananchi waliweka stop order mahakamani na wakavunjiwa kibabe. Kwa hiyo lazima Ilani iseme kupitia "Humanitarian grounds" kuwalipa fidia wananchi hawa, haswa ukizingatia operesheni iliyowavunjia nyumba zao ilikuwa ya kibaguzi. Kule Mwanza hawakuvunjiwa kwa amri ya rais kuwa wale walimpa kura.
9. Ilani zieleze kuhusu kuwapa wananchi bunge Live kama haki yao, zieleze kuhusu kukuza na kutetea demokrasia, freedom of press na maoni.
10. Ilani zisisahau Maji ya kunywa na salama, Afya za wananchi, Miundo mbinu, Ulinzi na usalama wa raia, Ilani lazima zieleze kuhusu namna zitakavyodeal na watu wasiojulikana, Zieleze kuhusu kuchunguza upotevu wa watu uliotokea katika kipindi cha utawala huu
Hayo ni baadhi tu ya mambo ambayo naamini yakiwekwa vizuri basi wananchi watawaeleweni vizuri sana!