ACT Wazalendo: Serikali inaziba masikio vilio vya wananchi ugumu wa maisha

ACT Wazalendo: Serikali inaziba masikio vilio vya wananchi ugumu wa maisha

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Chama cha ACT Wazalendo kimechukizwa na ugumu wa maisha unaowakabili wananchi kutokana na kupanda kwa bei ya bidhaa, utitiri wa kodi, tozo, ushuru na mazingira magumu ya kujipatia kipato.

Wakakizungumza kutoka maeneo mbalimbali ya nchi wanakoendelea na ziara ya Chama viongozi wameeleza kusikitishwa kuona Serikali ya Chama cha Mapinduzi haishtushwi, haijali na wala haijihangaishi kutatua matatizo na vikwazo vinavyowasukuma na kuwakandamiza wananchi kwenye lindi la umaskini. Badala ya serikali ya CCM kupambana na umasikini, Serikali inapambana na masikini. Inasikikitisha. CCM wamechoka tuwaondoe madarakani!

Msisitizo huu umetolewa katika ziara ya viongozi iliyoanza juzi tarehe 22 Julai 2024, katika mikoa ya Mwanza, Dodoma, Simiyu, Kigoma na Ruvuma. Katika kuelezea hali hiyo, Kiongozi wa Chama Ndg. Dorothy Manka Semu akiwa Kondoa Mjini amesema;

“Kupanda kwa gharama za maisha kumeathiri uwezo wa wananchi kupata mahitaji ya msingi. Tunaona mafuta ya petroli na diseli kwa miaka mitatu imepaa sana kutoka wastani wa bei ya shilingi 2,040/= mwaka 2021 hadi kufikia bei ya 3,270/= kwa Dodoma. Nauli za mabasi zimepanda na mbolea nazo hazikamatiki, ruzuku kwenye mbolea haiwafikii wakulima.”

Kiongozi wa Chama amesema suala la gharama kubwa linawaingiza wananchi kwenye umaskini kwa sababu wananchi wanashindwa kununua chakula, kugharamia afya, maji na umeme. ‘’Wananchi wanapaswa kuonesha hasira zao kwa kukikataa chama tawala na kujiunga na ACT Wazalendo,’’ alisisitiza.

Naye, Makamu Mwenyekiti Bara Ndg. Isihaka Mchinjita akizungumza kutoka jimbo la Madaba mkoani Ruvuma amesema wananchi wa Ruvuma wanapitia ugumu wa maisha kutokana na kupanda kwa bei ya mbolea tangu mwaka 2021. Ameeleza kuwa usambazaji wa mbolea za ruzuku kwa wakulima hauwanufaishi wakulima walio wengi, hivyo kuwafanya wakulima kushindwa kuzalisha na hatimaye kuingia katika umasikini.

“Tunafahamu kuwa kilio chenu kikubwa ni kuona mnaweza kuipata mbolea kwa wakati, kwa bei nafuu na yenye ubora. Serikali ya CCM inawahadaa kuwa inaweka ruzuku lakini wengi wenu hamjapata mbolea ya ruzuku. Na mwaka huu hali ni mbaya zaidi. Gharama za uzalishaji zimekuwa juu na bei ya mahindi imezidi kuporomoka,” amesema Mchinjita.

Ndg. Mchinjita aliendelea kuonesha namna gani sera na mienendo ya serikali inavyowadumaza watu wa mikoa ya kusini. “Bei ya mahindi wanayouza wakulima wa Madaba na takribani Ruvuma kote ni Shilingi 370/= hadi 400/= kwa kilo. Hivyo basi, mkulima wa mahindi Ruvuma anapaswa kuuza kilo kumi (10) za mahindi ili kupata kilo moja ya sukari. Hali hii inawaumiza sana na kuwadumaza wananchi wa Ruvuma.’’

Amesema wakati wananchi wanaendelea kufukarika, serikali inajinasibu kujihusisha na umasikini wa wananchi kwa kueleza kununua mahindi kutoka kwa wakulima. Ukweli hata hivyo ni kuwa, serikali kwa makusudi kabisa, inacheza michezo na watu wa kati, madalali, kwa kujichelewesha kununua mazao na hivyo kuwakuta wakulima wameshauza mazao yao kwa watu wa kati kutokana na dhiki zao walizopandikiziwa na CCM.

Hivyo, wakulima hawa wanajikuta wanabaki kila siku katika laana ya dhiki juu ya dhiki; ilihali watu wachache – watu wa kati na watu wa serikalini – ambao hata sio waliovuja jasho katika uzalishaji wa mazao hayo, ndio wanaoneemeka.

Amesema hali hiyo ndiyo inaifanya Mkoa wa Ruvuma ambao unasifika kwa kuwa tegemeo la nchi katika kuzalisha Chakula ukiwa ni miongoni mwa mikoa iliyokithiri kwa udumavu na ikitajwa kuwa mkoa wa tano wenye udumavu, ukiwa na aslimia 35 ya watu wanaoshindwa kula mlo kamili. Na hivyo kusisitiza kwamba wananchi hawapaswi kuendelea kushuhudia maisha yao yanaendelea kuangamizwa na viongozi wasiojali maisha yao.

Wilayani Busega, mkoani Simiyu, Katibu Mkuu wa Chama, Ndg. Ado Shaibu amesisitiza kuwa, kuporomoka kwa bei ya pamba, kutoka kuuzwa shilingi 2,000/= mwaka 2022 mpaka kuuzwa shilingi 1,060/= mwaka jana, kumeongeza maumivu na hali ngumu.

Kiongozi huyo alieleza zaidi kuwa suala la ugumu wa maisha linawatesa zaidi watu wa Simiyu kuliko maeneo mengine mengi; kwani mkoa huo unashika nafasi ya pili kwa kiwango cha juu cha umasikini na utegemezi nchini.

Katika kueleza zaidi kuhusu hali ya umasikini nchini, Kiongozi wa Chama mstaafu, Ndg. Zitto Kabwe, naye akiwa mkoani Kigoma aliangazia namna gani tatizo la umasikini ni sugu na limewashinda CCM, ambapo alieleza kuwa janga hilo ni kuu katika mkoa wa Kigoma na nchini kote.

Ndugu Zitto alieleza kuwa, “…kuna mikoa 7 hapa Tanzania, zaidi ya 30% ya wananchi wake wanaishi chini ya mstari wa umasikini, yaani hawana uwezo wa kupata na kutumia Tshs 1,700/= kila siku. Mikoa hii tumeiita Mikoa ya Ukanda wa Umasikini - Kigoma, Tabora, Rukwa, Katavi, Shinyanga, Kagera na Geita.”

Katika ziara hiyo, viongozi wa ACT Wazalendo wanaendelea kutoa wito kwa wananchi waliochoshwa na kadhia na fedheha za umasikini unaopaliliwa na serikali na sera mbaya za CCM wachukue hatua ya kujiunga na ACT Wazalendo, ili kuleta mabadiliko yatakayojenga uchumi unaozalisha na kulinda fursa nyingi za ajira na shughuli za uhakika za kujiingizia kipato; maisha yenye staha na nafuu; huduma bora za jamii zinazozingatia utu na usawa.


Imetolewa na;

Shangwe Ayo
Naibu Katibu Idara ya Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma
ACT Wazalendo
24 Julai, 2024.
 
Chama cha ACT Wazalendo kimechukizwa na ugumu wa maisha unaowakabili wananchi kutokana na kupanda kwa bei ya bidhaa, utitiri wa kodi, tozo, ushuru na mazingira magumu ya kujipatia kipato...
Gen Z wanaandamana tarehe 5.8.2024 tunataka kuwaona na ninyi ndani yao kama mnakerwa kweli
 
Act wazalendo.jpg

Chama cha ACT Wazalendo kimechukizwa na ugumu wa maisha unaowakabili wananchi kutokana na kupanda kwa bei ya bidhaa, utitiri wa kodi, tozo, ushuru na mazingira magumu ya kujipatia kipato.

Wakizungumza kutoka maeneo mbalimbali ya nchi wanakoendelea na ziara ya Chama viongozi wa chama hicho wameeleza kusikitishwa na kuona serikali haishtushwi, haijali na wala haijihangaishi kutatua matatizo na vikwazo vinavyowasukuma na kuwakandamiza wananchi kwenye lindi la umaskini.

Badala ya serikali ya CCM kupambana na umasikini, Serikali inapambana na masikini. Inasikikitisha. CCM wamechoka tuwaondoe madarakani! Msisitizo huu umetolewa katika ziara ya viongozi iliyoanza juzi tarehe 22 Julai 2024, katika mikoa ya Mwanza, Dodoma, Simiyu, Kigoma na Ruvuma. Katika kuelezea hali hiyo, Kiongozi wa Chama Dorothy Semu akiwa Kondoa Mjini alisema; “Kupanda kwa gharama za maisha kumeathiri uwezo wa wananchi kupata mahitaji ya msingi. Tunaona mafuta ya petroli na diseli kwa miaka mitatu imepaa sana kutoka wastani wa bei ya shilingi 2,040/= mwaka 2021 hadi kufikia bei ya 3,270/= kwa Dodoma. Nauli za mabasi zimepanda na mbolea nazo hazikamatiki, ruzuku kwenye mbolea haiwafikii wakulima.”

Kiongozi huyo wa chama alisema suala la gharama kubwa linawaingiza wananchi kwenye umaskini kwa sababu wananchi wanashindwa kununua chakula, kugharamia afya, maji na umeme.

‘’Wananchi wanapaswa kuonesha hasira zao kwa kukikataa chama tawala na kujiunga na ACT Wazalendo,’’ alisisitiza.

Naye, Makamu Mwenyekiti Bara, Isihaka Mchinjita akizungumza kutoka Jimbo la Madaba mkoani Ruvuma amesema wananchi wa Ruvuma wanapitia ugumu wa maisha kutokana na
kupanda kwa bei ya mbolea tangu mwaka 2021.

Ameeleza kuwa usambazaji wa mbolea za ruzuku kwa wakulima hauwanufaishi wakulima walio wengi, hivyo kuwafanya wakulima kushindwa kuzalisha na hatimaye kuingia katika umasikini.

“Tunafahamu kuwa kilio chenu kikubwa ni kuona mnaweza kuipata mbolea kwa wakati,kwa bei nafuu na yenye ubora. Serikali ya CCM inawahadaa kuwa inaweka ruzuku lakini wengi wenu hamjapata mbolea ya ruzuku. Na mwaka huu hali ni mbaya zaidi. Gharama za uzalishaji zimekuwa juu na bei ya mahindi imezidi kuporomoka,” amesema Mchinjita.

Mchinjita aliendelea kuonesha namna gani sera na mienendo ya serikali inavyowadumaza watu wa mikoa ya kusini. “Bei ya mahindi wanayouza wakulima wa Madaba na takribani Ruvuma kote ni Shilingi 370/= hadi 400/= kwa kilo. Hivyo basi, mkulima wa mahindi Ruvuma anapaswa kuuza kilo kumi (10) za mahindi ili kupata kilo moja ya sukari. Hali hii inawaumiza sana na kuwadumaza wananchi wa Ruvuma.’’

Amesema wakati wananchi wanaendelea kufukarika, serikali inajinasibu kujihusisha na umasikini wa wananchi kwa kueleza kununua mahindi kutoka kwa wakulima.

Ukweli hata hivyo ni kuwa,serikali kwa makusudi kabisa, inacheza michezo na watu wa kati, madalali, kwa kujichelewesha kununua mazao na hivyo kuwakuta wakulima wameshauza mazao yao kwa watu wa kati
kutokana na dhiki zao walizopandikiziwa na CCM.

Hivyo, wakulima hawa wanajikuta wanabaki kila siku katika laana ya dhiki juu ya dhiki; ilihali watu wachache – watu wa kati na watu wa serikalini – ambao hata sio waliovuja jasho katika uzalishaji wa mazao hayo, ndio wanaoneemeka.

Amesema hali hiyo ndiyo inaifanya Mkoa wa Ruvuma ambao unasifika kwa kuwa tegemeo la nchi katika kuzalisha Chakula ukiwa ni miongoni mwa mikoa iliyokithiri kwa udumavu na ikitajwa kuwa mkoa wa tano wenye udumavu, ukiwa na aslimia 35 ya watu wanaoshindwa kula mlo kamili. Na hivyo kusisitiza kwamba wananchi hawapaswi kuendelea kushuhudia maisha yao yanaendelea kuangamizwa na viongozi wasiojali maisha yao.

Wilayani Busega, mkoani Simiyu, Katibu Mkuu wa Chama, Ado Shaibu amesisitiza kuwa, kuporomoka kwa bei ya pamba, kutoka kuuzwa shilingi 2,000/= mwaka 2022 mpaka kuuzwa shilingi 1,060/= mwaka jana, kumeongeza maumivu na hali ngumu.

Kiongozi huyo alieleza zaidi kuwa suala la ugumu wa maisha linawatesa zaidi watu wa Simiyu kuliko maeneo mengine mengi; kwani mkoa huo unashika nafasi ya pili kwa kiwango cha juu cha umasikini na utegemezi nchini.

Katika kueleza zaidi kuhusu hali ya umasikini nchini, Kiongozi wa Chama mstaafu, Zitto Kabwe, naye akiwa mkoani Kigoma aliangazia namna gani tatizo la umasikini ni sugu na limewashinda CCM, ambapo alieleza kuwa janga hilo ni kuu katika mkoa wa Kigoma na nchini kote. ZITTO ATEMA CHECHE, TATIZO LA UMASKINI SUGU LIMEWASHINDA CCM

Zitto alieleza kuwa, “…kuna mikoa 7 hapa Tanzania, zaidi ya 30% ya wananchi wake wanaishi chini ya mstari wa umasikini, yaani hawana uwezo wa kupata na kutumia Tshs 1,700/= kila siku. Mikoa hii tumeiita Mikoa ya Ukanda wa Umasikini - Kigoma, Tabora, Rukwa, Katavi, Shinyanga, Kagera na Geita.”

Katika ziara hiyo, viongozi wa ACT Wazalendo wanaendelea kutoa wito kwa wananchi waliochoshwa na kadhia na fedheha za umasikini unaopaliliwa na serikali na sera mbaya za CCM wachukue hatua ya kujiunga na ACT Wazalendo, ili kuleta mabadiliko yatakayojenga uchumi unaozalisha na kulinda fursa nyingi za ajira na shughuli za uhakika za kujiingizia kipato; maisha yenye staha na nafuu; huduma bora za jamii zinazozingatia utu na usawa.


Chanzo: Nipashe
 
Hawa act si walisema hawatamsena vibaya mama

Wakasema hawata weka mgombea wa uraisi mpaka 2030

Wakamalizia kwa kusema mama anaupiga mwingi

Sasa imekuwaje tena??
 
Navyojua ACT na CCM wameshirikiana kuunda serikali iliyopo. Kwa hiyo ACT nao wanamchango kwenye kufanya maisha yetu yawe magumu
 
Huyu Zitto sasa ndio atasikika mpaka! Mnafki namba moja.
 
Back
Top Bottom