LGE2024 ACT Wazalendo: Tumebaini mapungufu makubwa yanayoathiri ufanisi, uhuru na kutendeka haki katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa

LGE2024 ACT Wazalendo: Tumebaini mapungufu makubwa yanayoathiri ufanisi, uhuru na kutendeka haki katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2012
Posts
6,067
Reaction score
10,938
MAPUNGUFU MAKUBWA UANDIKISHAJI WAPIGAKURA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA

Chama cha ACT Wazalendo kinafuatilia kwa karibu mwenendo wa mchakato unaoendelea wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa kulingana na ratiba iliyotolewa na Waziri mwenye dhamana ya TAMISEMI. Tangu kuanza kwa mchakato wa uchaguzi huo, tumebaini mapungufu makubwa yanayoathiri ufanisi, uhuru na kutendeka haki katika uchaguzi huo. Mapungufu hayo ni kama yafuatayo;
a) Ukosefu wa Uratibu Baina ya TAMISEMI, Halmashauri na Wadau wa Uchaguzi

Tathmini yetu inaonesha kuwa tangu kuanza kwa mchakato wa uchaguzi huu, hakuna uratibu unaoelewaka baina ya Msimamizi Mkuu wa Uchaguzi kwa maana ya Waziri wa TAMISEMI, Halmashauri amba oni Wasimamizi wa Ngazi za chini na Wadau wa uchaguzi hasa vyama vya siasa.

Hali hii imepelekea kila Halmashauri kuwa na utaratibu na mkondo wake wa namna inavyoendesha zoezi la uchaguzi. Hakuna mtiririko juu ya utoaji wa taarifa na maelekezo kuhusu utaratibu mzima wa Uchaguzi, kila ngazi na kila eneo Wasimamizi au Wasimamizi wasaidizi wa Uchaguzi huu wanatoa taarifa wajuavyo wao na kwa muda wanaoupanga wao. Pamoja na kwamba TAMISEMI wametoa Kanuni na Mwongozo kuhusu mchakato mzima wa Uchaguzi lakini katika zoezi la Vyama vya Siasa kutoa Mawakala wa Uandikishaji wa Wapiga Kura imeishia kuelezwa kuwa ni haki ya vyama kupeleka Mawakala katika vituo vya kuandikisha Wapiga Kura tu.
b) Taarifa Kutoka kwa Wasimamizi wa Uchaguzi Kutolewa kwa Dharura

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa, zoezi la uandikishaji wapigakura linaanza tarehe 11 hadi 20 Oktoba, 2024. Hata hivyo, taarifa za kutakiwa kuwasilisha mawakala wa usimamizi wa uandikishaji kutoka kwa wasimamizi wa uchaguzi ngazi ya Halmashauri kwenda kwa viongozi wetu wa Chama ngazi za chini zimetolewa siku moja kabla ya kuanza zoezi.

  • Bagamoyo, katika Kata ya Yombo kwa mfano Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi amewaita viongozi wa vyama na ametoa taarifa ya kikao tarehe 9 Oktoba 2024 asubuhi na kikao ni tarehe 9 Oktoba 2024 saa tano asubuhi kwamba vyama vipeleke orodha ya Mawakala siku hiyo hiyo mchana ili tarehe 10 waweze kuapishwa.​
  • Baadhi ya maeneo, Viongozi wetu wametakiwa kupeleka majina ya Mawakala wakiambatanisha na nakala ya picha za pasipoti kwa kila wakala ili kuwatambua, kinyume kabisa na miongozo na Kanuni ya Uchaguzi. Mfano; Kibiti eneo la delta.​
c) Uapishwaji wa Mawakala wa Uandikishaji Wapigakura

Tumepokea taarifa katika maeneo mengi wasimamizi wa uchaguzi ngazi ya Halmashauri wameitisha zoezi la viapo vya mawakala kufanyika katika ofisi za Halmashauri husika. Kwa jiografia ya nchi yetu, maeneo mengi yako mbali na Halmashauri. Hivyo, ni ngumu kwa mawakala kufika kwa ajili ya viapo. Utaratibu huo utawaacha mawakala bila viapo na ikiwa hawataapishwa maana yake hawatakuwa na sifa za kusimamia zoezi la uandikishaji.

  • Newala, Viongozi wetu wa Chama wametakiwa kuwapeleka Mawakala wote Newala Mjini kwenda kuapishwa ambapo baadhi ya maeneo yana zaidi ya Kilometa 70 mfano yale yanayopakana na Msumbiji.​

MAPENDEKEZO YETU
a) Uratibu wa Kitaifa Baina ya TAMISEMI na Wadau
TAMISEMI iimarishe uratibu wa mchakato wa uchaguzi baina yake na Halmashauri na wadau wa uchaguzi hasa vyama vya siasa. Zoezi hili linahitaji mawasiliano na uratibu wa karibu baina ya mamlaka na wadau. Ukosefu wa uaratibu unaoeleweka utatafsiriwa kuwa ni hujuma za makusudi katika uchaguzi.
b) Mawakala Waapishwe Kwenye Vituo vya Kupigia Kura Badala ya Halmashauri
Utaratibu wa kuapishwa mawakala katika Halmashauri hauna ufanisi na hauwezekani. TAMISEMI itoe maelekezo mawakala wote waapishwe katika vituo vya kupigia kura.
c) Taarifa na Elimu itolewe kwa kiwango cha kuridhisha
Bado hatuoni jitihada za kutosha za utoaji wa taarifa na elimu kuhusu uchaguzi wa serikali za mitaa. Tunatoa rai taarifa na elimu itolewe kwa wakati na kwa kiwango kinachohitajika.
ACT 1.jpg
ACT 2.jpg
 
Back
Top Bottom