The Sheriff
JF-Expert Member
- Oct 10, 2019
- 747
- 2,112
Tamko la ACT Wazalendo kuhusu ukiukwaji wa Haki za Binadamu limetolewa leo katika mkutano na Waandishi wa Habari na Mkuu wa Idara ya Haki za Binadamu na Vyombo vya Uwakilishi wa Wananchi wa chama hicho, Mbarala Maharagande, leo Desemba 1, 2024
WANACHAMA WETU 200 WANAISHI PORINI KWA VITISHO VYA POLISI
Kama mnavyofahamu, jumatano wiki hii tulikuwa na uchaguzi wa serikali za mitaa, na sote tumeshudia uchafuzi mkubwa wa uchaguzi huo, matumizi makubwa ya Jeshi la Polisi likiisaidia CCM iweze kushinda. Jeshi la Polisi limetumika moja kwa moja pamoja na wanaoitwa wasimamizi wa uchaguzi ambao wengi wao ni makada wa CCM…
…tumepokea taarifa kutoka Kigoma kuwa vijana wetu zaidi ya 200 wapo porini wakihofia maisha yao kutokana na Jeshi la Polisi kutumia nguvu kubwa na kuwakamata wanachama wetu zaidi ya 20 ambao wapo mahabusu, kati yao wanawake wakiwa saba.
Kutoka Ludewa kwenye Kijiji cha Mapogoro, Kata ya Milo, Tarafa ya Liganga, wanachama wetu wanaishi maporini kutokana na vitisho vya CCM kupitia Jeshi la Polisi wabnafanya kwa wagombea wetu walioporwa ushindi wao na kuvurugwa katika uchaguzi. Miongoni mwao kesho Jumatatu wametakiwa warejee Polisi kwenda kuripoti, akiwemo Zakaria Sangijo Lugembe.
Vitisho hivyo vimeendelea katika kila kona ya nchi yetu.
TUNAAMINI ABDUL NONDO ANASHIKILIWA NA VYOMBO VYA DOLA
Leo saa 11 alfajiri Mwenyekiti wetu wa Ngome ya Vijana, Abdul Nondo, amekamatwa na watu watatu wanaosadikiwa kuwa ni Askari wa Polisi… Haya mabo na matukio mfano wa haya yanafanywa na watu wabaiojua nini ambacho wanakifanya, kwa lengo la kutisha watu kwa hofu ya uchaguzi uliovurugwa…
…tumetoa taarifa kwa Jeshi la Polisi Kituo cha Magufuli, wamechukua maelezo na wametupa muda kuona ni kituo gani anashikiliwa. Mpaka sasa nazungumza hatujapata taarifa zozote za Mwenyekiti wetu yupo katika kituo gani cha polisi hapa Dar es Salaam.
Tunatoa wito kwa Jeshi la Polisi na IGP kama tulivyotoa taarifa yetu ya awali kuoitia press release ambayo tuliitoa mapema asubuhi ya leo baada ya kupata taarifa za kuchukuliwa kwa Mwenyekiti wetu.
Tunataka Jeshi la Polisi kupitia IGP pamoja na kwamba nao wametoa taarifa ya kuonesha kwamba wanaendelea kufuatilia, lakini sisi tuna uthibitisho na tunaamini kuwa mwenyekiti wetu yupo kwenye mikono ya vyombo vya dola. Kama sio wao Jeshi la Polisi, basi ni maafisa wa usalama ndiyo waliofanya tukio hilo.
Kwahiyo, wamuachie Mwenyekiti wetu au wamfikishe kwenye vyombo vya sheria ili aweze kujitetea kama atakuwa na kesi ya kujibu kwa kosa walilomkamatia.
Ahsanteni sana
Pia soma: Dar: Abdul Nondo amechukuliwa na Watu wasiojulikana katika mazingira ya utatanishi Kituo cha Mabasi cha Magufuli