ACT Wazalendo tunataka CAG afanye Ukaguzi maalum wa Fedha za Muungano

ACT Wazalendo tunataka CAG afanye Ukaguzi maalum wa Fedha za Muungano

Wiston Mogha

Senior Member
Joined
Feb 13, 2014
Posts
168
Reaction score
141
ACTwazalendo tunataka CAG afanye Ukaguzi maalum wa Fedha za Muungano, Mapato, Matumizi na Fedha zinazobakia, ili kubainisha mgao sahihi na fedha ambazo Zanzibar inastahiki kupata.

Naibu Waziri Kivuli wa Fedha
Shangwe Ayo

#Maumivuyanaendelea
#Bajetiyawalanchi

d9b1092a-074d-4706-9c41-c4ff5217e3dd.jpeg
 
Fedha za Muungano zinaendelea kutumika bila kujali haki na usawa wa pande zote mbili. @ACTwazalendo tunataka Serikali ifuate Katiba kwa kuanzisha Akaunti ya Pamoja ya Fedha kwa mujibu wa sheria na mapato ya Muungano yawekwe humo.

N/Waziri Kivuli wa Fedha
Shangwe Ayo

8954c037-51b9-424b-9f3a-45e64c624d08.jpeg
 
Bila kusau
matumizi ya fedha za mkopo kutoka nje ya nchi (2005 hadi 2024)

kwa kuzingatia malengo au mahitaji ya mkopo, riba ya mkopo, ufanisi wa mkopo, matumizi yaliyokusudiwa au yaliyopindishwa, na ufisadi au ufujaji
 
ACT waweke maelezo vizuri. Upande gani wanafikiri unafaidi zaidi hadi kupelekea wao (ACT) kuja na tamko hili.

Kwa hali ilivyo sasa, Zanzibar wanatumia pesa nyingi kuliko kiwango kilochopendekezwa na katiba/sheria.

*Madaraja ya juu (flyovers) yanajengwa kila pembe ya Zanzibar.
*Viwanja vya ndege vya kimataifa vinajengwa.
*Viwanja vya mpira vya kisiasa.
*Kila shule Zanzibar inabomolewa na kujengwa ya ghorofa.

Yote haya na mengine mengi yanafanywa kwa kodi ipi inayokusanywa huko Zanzibar? Samia anatuibia.
 
Zanzibar wanachangia ninii mfumo huu WA Muungano? Kwa miaka 60 Zanzibar wamechangia kiasi Gani?
 
Kwa ujumla katika awamu hii, pesa ya Tanganyika inatumika kuijenga Zanzibar. Raia anaitumia nafasi yake kuinufaisha Zanzibar kinyume na makubaliano.
 
ACT waweke maelezo vizuri. Upande gani wanafikiri unafaidi zaidi hadi kupelekea wao (ACT) kuja na tamko hili.

Kwa hali ilivyo sasa, Zanzibar wanatumia pesa nyingi kuliko kiwango kilochopendekezwa na katiba/sheria.

*Madaraja ya juu (flyovers) yanajengwa kila pembe ya Zanzibar.
*Viwanja vya ndege vya kimataifa vinajengwa.
*Viwanja vya mpira vya kisiasa.
*Kila shule Zanzibar inabomolewa na kujengwa ya ghorofa.

Yote haya na mengine mengi yanafanywa kwa kodi ipi inayokusanywa huko Zanzibar? Samia anatuibia.

unauhakika gani kama hayo uliyoyataja hela inatoka Tanganyika?
 
Hapa Anakumbukwa Sana Mbunge Wa Zamani Wa Nkasi, Ally Kessy Yule Zilikuwa Hoja Zinazohusu Zanzibar Anazikimbiza Mbali Sana Tena Kwa Kishindo
 
Back
Top Bottom