Pre GE2025 ACT Wazalendo wafungua mashitaka dhidi ya Mkuu wa Wilaya kwa kukamata na kupiga Watu wakati wa Uandikishaji Wapiga Kura Zanzibar

Pre GE2025 ACT Wazalendo wafungua mashitaka dhidi ya Mkuu wa Wilaya kwa kukamata na kupiga Watu wakati wa Uandikishaji Wapiga Kura Zanzibar

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

upupu255

Senior Member
Joined
Sep 4, 2024
Posts
119
Reaction score
144
Chama cha ACT wazalendo kimeamua kuwashitaki viongozi wanaotumia vibaya madaraka yao kwa kukamata watu kinyume na sheria na kuwapiga pamoja na kuingia zoezi la uandikishaji wapga kura linaloendelea Zanzibar.

Chini ya mpango huo wameanza kwa kufungua mashitaki dhidi ya mkuu wa wilaya ya magharibi B Sadija Juma Khamis ambaye anatuhumiwa kutoa amri kukamatwa kwa watu wawili katika vituo vya uandikishaji na kuwekwa ndani kituo cha polisi….ambao walipigwa na baadae kutibiwa hospitali.

Screenshot 2025-03-05 172405.png
Mpango huo umetangazwa na mwanasheria mkuu wa chama hicho Omar Said Shaaban alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwao Vuga Mkoa wa Mjini Magharibi.

Soma: Mchakato wa uandikishaji wa wapiga kura kwa awamu ya pili waendelea Zanzibar. Changamoto "ndogondogo" zajitokeza!

Mwanasheria huyo amesema kwamba wakili anayesimamia shauri hilo tayari ameshaandika barua ya indhari ya kushitakiwa kwa mkuu wa wilaya na kukabidhiwa sheha wa shehia yake ambapo ametakiwa kujibu ndnai ya siku saba kabla ya kesi kufikishwa mahakamani.

Amesema kwamba katika kesi hiyo kila mdai atataka kulipwa shilingi milioni mia mbili kila mmoja na kesi hiyo imefunguliwa mkuu wa wilaya kama yeye binafsi na sio serikali na awepo kwenye madaraka au asiwepo kesi inaendelea pale pale.

Omar amesema hata kama mkuu wa wilaya hatojibu barua hiyo utaratibu wa kumfikisha mahakamani utaendelea kufanyika kama kawaida pamoja na viongozi wengine ambao wamefanya vitendo kama hivyo tangu zoezi la uandikishaji lilipoanza kufanyika Febuari na kuanzia katika wialaya za Pemba.

Amesema kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi ya Zanzibar kuna watu ambao wameorodheshwa wanaotakiwa kuwepo katika kituo akiwemo afisa uandikishaji, mawakala wa vyama vya siasa, askari polisi na afisa wa usalama na masheha lakini kumejitokeza kitendo cha wakuu wa wilaya na mikoa kwa kutumia nafasi zao kama wenyeviti wa kamati za siasa wamekuwa wakenda katika vituo vya uchaguzi wakiwa wameambatana na askari wa vikosi vya SMZ na kutoa amari za watu kukamatwa, kupigwa na kuwapeleka kwenye vituo vya polisi kabla ya kuachiwa na kufunguliwa mashtaka.

“Wakuu wa wilaya na mikoa wasigeuze vituo vya polisi maghala au stoo za kutesa watu, haiwezekani umkamate mtu kwa kutoa amari na kumpekeka polisi bila ya kosa na baadae anaachiwa bila ya kufunguliwa mashitaka yoyote jambo hili ni
 
Alafu mnashiriki uchaguzi
Mtapigwa sana tu 😄

Ova
 
Back
Top Bottom