LGE2024 ACT Wazalendo: Wakala wetu wa Bunda ameshambuliwa na kuumizwa kisha amepelekwa Polisi, wanadai amefanya fujo

LGE2024 ACT Wazalendo: Wakala wetu wa Bunda ameshambuliwa na kuumizwa kisha amepelekwa Polisi, wanadai amefanya fujo

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
WhatsApp Image 2024-11-28 at 08.36.17_381cb195.jpg
Chama cha ACT Wazalendo kimesema Wakala wao katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, TINGA TOGORO KERANGA kutoka Kata ya Hunyari, Kijiji cha Mariwanda, Kituo cha Kilimani alifanyiwa fujo kwa kunyang'anywa karatasi za Kura na Wakala wa CCM ambaye alizichana baada ya kuona kuwa Wakala wa ACT Wazalendo anazo kura nyingi kuliko wakala wengine.

Jambo hilo lilisababisha kuitwa na Aaskari wa Jeshi la Polisi na kukamatwa na kupelekwa Ofisini na baadaye akapelekwa Polisi Bunda.

Akifafanua kuhusu kilichotokea, Mjumbe wa ACT Bunda, Mayunga Kilanga amesema "Walimvamia Keranga wakaanza kumshambulia kisha wakapiga simu Polisi wakidai yeye ndiye kasababisha fujo, wamemkamata na kumpeleka kituoni tangu jana (Novemba 27, 2024). Tunawasiliana na ACT Taifa ili kuoata Wanasheria wa kusimamia suala lake.

"Walipomchukua huku nyumba wakamtangaza Mgombea wa CCM kuwa mshindi bila ya upande wa pili kusaini fomu ya makubaliano."

===============​
UPDATES...

ACT WATAKA UCHAGUZI URUDIWE KATA YA HUNYARI

Mjumbe wa ACT Bunda, Mayunga Kilanga amesema "Hatimaye Keranga amefanikiwa kutoka asubuhi hii, Polisi wamemruhusu na kumtaka arejee kesho kituoni hapo, mpango uliopo kwa sasa ni kumpeleka Hospitali kwa kuwa bado ana maumivu, walimuumiza sana walipomshambulia.

"Baada ya hapo tuna mpango wa kukata rufaa uchaguzi urudiwe kwa kuwa Wakala wetu aliondolewa kihuni na hakukuwa na haki iliyotendeka, tumeshaanza mchakato ili tuhakikishe Uchaguzi unarudiwa.
 
Back
Top Bottom