Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,869
- 4,877
Wakuu,
Haya jamani mliokuwa mnasema kuwa ACT Wazalendo ni CCM B mna salamu zenu hapa.
Nimeona hivi karibuni Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Jimbo la Momba, Himid Yaled Siwale amesimamishwa uongozi kutokana na video inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii, akipongeza kuwa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ulikwenda vizuri,
Kwenye barua iliyosainiwa na Katibu Mkuu wa chama hicho, Ado Shaibu, Kiongozi huyo wa Jimbo la Momba amepewa siku tano ajieleze kwa nini asiondolewe kwenye nafasi yake ya uenyekiti moja kwa moja kwa kukiuka msimamo wa chama hicho.
Soma pia: Songwe: Ado Shaibu wa ACT Wazalendo atangaza kufuta uanachama viongozi wote wasaliti ndani ya chama hicho
Ikumbukwe kuwa tarehe 29 Novemba, Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo Dorothy Semu aliweka bayana kuwa chama hicho hakikubaliani na matokeo ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika Novemba 27, 2024 kwa sababu mchakato mzima wa uchaguzi huo ulitawaliwa na wizi wa kura, kura bandia na vitendo vingine vilivyokusudia kukibeba Chama cha Mapinduzi (CCM).
Source Jambo TV