Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,108
- 10,191
Maneno yanayoendelea mtandaoni ni mengi ila inaonyesha Membe kakaza hawezi kuruhusu kuacha kujaribu kutetea ndoto yake ya kuwa rais.
Awali Membe alijiamini kuwa na watu wengi nyuma yake ambao angehama nao, lakini akajikuta ameondoka mwenyewe, wale wachache kutoka CUF na CCM waliojiunga na ACT Lindi na Mtwara, walirudisha kadi kwa mama Samia na kujiunga na CCM.
Hii inaonyesha hata wachache walioamini kuwa kweli ana nguvu wameona hana nguvu za hivyo. ACT ni tofauti na CCM, kwa kuwa Membe sio Mwenyekiti wa ACT ila ni Mshauri, maamuzi yanabaki kuwa ya Mwenyekiti, Mshauri sio lazima ushauri wake ukubalike, sasa hapo utaona kuwa Membe alikuwa anavumiliwa tu.
Lakini je, wakiamua kumvua uanachama Membe kwa hali ya sasa, je ACT Itakuwa na hasara yoyote?
Hujuma dhidi ya Membe zilianza kitambo.
Picha linaanza ule wimbo wa Baba Levo hausikiki, wanaimbaga: "Jamani Membe huyoo, Membe huyooo'" hausikiki nikaona mh! kuna kitu hapa.