Uchaguzi 2020 ACT Wazalendo wapo tayari kuunga mkono CHADEMA, Membe bado hajajibu suala kama atakubaliana

Uchaguzi 2020 ACT Wazalendo wapo tayari kuunga mkono CHADEMA, Membe bado hajajibu suala kama atakubaliana

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
ACT-Wazalendo ipo tayari ubia na CHADEMA

KIONGOZI Mkuu wa Chama cha ACT- Wazalendo, Zitto Kabwe, amesema chama chake kipo tayari kushirikiana na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuungana mkono kwa wagombea wanaokubalika kwenye majimbo ili waweze kuibuka na ushindi.

zitto0.jpg


Alitoa ufafanuzi huo baada ya ombi la mgombea urais wa CHADEMA, Tundu Lissu, kuachiwa upande wa Tanzania Bara kwa kuwa ndiyo chama chenye misuli ya kushindana na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Akizungumza na wahariri na waandishi waandamizi wa vyombo mbalimbali vya habari nyumbani kwake jijini Dar es Salaam Alhamisi iliyopita, Lissu alisema kuwa tayari chama hicho kimeshakubali kumwachia mgombea urais wa ACT-Wazalendo, visiwani Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad.

Zitto aliiambia Nipashe wakati akitoa msimamo wa chama hicho kuwa: “Tunaendelea kuzungumza na CHADEMA kuhusu kushirikiana. Ninaamini kuwa tutakubaliana majimbo ya kuachiana na pia mgombea mmoja wa upinzania wa urais wa kupigiwa kura na wananchi.”

Kwa upadne wake Lissu alisema CHADEMA tayari imeshatangaza hadharani kuwa kitamuunga mkono mgombea urais wa Zanzibar wa ACT-Wazalendo, kwa kuwa ndiye anayekubalika na anaweza kumshinda mgombea wa CCM.

Kutokana na hali hiyo, Lissu alisema kwa haraka kwa upande wa Bara chama na mgombea anayeweza kuishinda CCM ni yeye (Lissu) na kukiomba ACT-Wazalendo kufikiria suala hilo na kukubali kumuunga mkono.

“Mazungumzo na ACT-Wazalendo hayajafa ila tumesema Maalim Seif ndiye anaweza kuishinda CCM Zanzibar na ndiyo tutawaunga mkono asilimia 100, sisi tunaweza kuokoteza kura, lakini hatutaweza kuishinda CCM Zanzibar, wagombea wetu tumewataka wamuunge mkono, si msimamo wa Lissu bali uongozi wa CHADEMA,” alifafanua.

“Ukiangalia Bara kwa macho angavu anayeweza kuishinda CCM ni CHADEMA, tumependekeza kwa wenzetu watuachie upande wa Bara, hatusemi waachie kila kitu bali yale maeneo ambayo watashinda waendelee, tusigombee kiti kama abiria wa ‘Titanic’, kikubwa tushinde uchaguzi Bara na Zanzibar halafu tutakaa tuzungumze,” alibainisha.

Nipashe ilimtafuta mgombea urais wa ACT- Wazalendo, Bernard Membe, kupata msimamo wake kuhusu suala hilo, simu yake haikupatikana na alivyotumiwa ujumbe mfupi kupitia WhatsApp haukujibiwa.

NIPASHE
 
Sishauri CHADEMA kuungana na ACT, bali wanaweza kuachiana majimbo kadhaa sehemu mmoja mwenye nguvu. Huyo Membe akikubali kuungana, baadae atatumika na CCM kuchukua taarifa za ndani za upinzani na kuanza kuuhujumu. Hakuna kuwa na ushirikiano na hao wanaccm wachafu, tumeona kwa Lowassa na Sumaye.
 
Sishauri CHADEMA kuungana na ACT, bali wanaweza kuachiana majimbo kadhaa sehemu mmoja mwenye nguvu. Huyo Membe akikubali kuungana, baadae atatumika na ccm kuchukua taarifa za ndani za upinzani na kuanza kuuhujumu. Hakuna kuwa na ushirikiano na hao wanaccm wachafu, tumeona kwa Lowassa na Sumaye.
Sasa ndohivyo wakubwa wanakaribia kufikia maelewano, wewe kapuku utafanya nini😂? Yani watu wasichukue hela kisa wewe umeshauri😂😂😂.
 
Magufuli kaungana na Tlp na cheyo na Lipumba hata Act waungane na ccm, sisi Chadema tunawapiga kura mil 20. Waliojiandika kuanzia 18-30
 
Bado CUF tu
Mwambieni kuwa makaburu wa Afrika kusini waliijenga S.A kama ULAYA, lakini haikuwafanya "WASAUZI" wawapende makaburu kwa UKATILI wao.

Mnamo mwaka 1994 makaburu waliondolewa madarakani, kwahiyo TUDARAJA 'twake' tusimpe uhalali wa kulazimisha KUTAWALA watu kwa MKONO WA CHUMA.
 
Mwambieni kuwa makaburu wa Afrika kusini waliijenga S.A kama ULAYA, lakini haikuwafanya "WASAUZI" wawapende makaburu kwa UKATILI wao.

Mnamo mwaka 1994 makaburu waliondolewa madarakani, kwahiyo TUDARAJA 'twake' tusimpe uhalali wa kulazimisha KUTAWALA watu kwa MKONO WA CHUMA.
Simoooo
 
Back
Top Bottom