Uchaguzi 2020 ACT- Wazalendo: Watakaoiba kura Mungu atawaadhibu

Uchaguzi 2020 ACT- Wazalendo: Watakaoiba kura Mungu atawaadhibu

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Mwenyekiti wa Ngome ya Wazee ya ACT-Wazalendo, Yassin Mohammed amesema, mwenyezi Mungu atawaadhibu watakaoshiriki wizi wa kura kwenye Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020.
Yassin ameyasema hayo leo Jumapili tarehe 27 Septemba 2020, kwenye uzinduzi wa kampeni za Mgombea Ubunge wa Kinondoni, Saed Kubenea katika Viwanja vya Buibui Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Mzee Yassin amesema, maombi yanayofanya na mtu aliyedhulumiwa hukubaliwa na mwenyezi Mungu haraka.

“Mtu yoyoye atakayedhulumu haki yetu awe ndani ya chama chetu au chama kingine au msimamizi wa uchaguzi mwenyezi Mungu atamuadhibu,” amesema Yassin.

Wakati huo huo, Yassin amewataka wananchi wa Kinondoni kutochagua viongozi wanaotokana na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kuwa hawaweki maslahi ya wananchi mbele badala yake wanailinda Serikali .
 
MWENYEKITI wa Ngome ya Wazee ya ACT-Wazalendo, Yassin Mohammed amesema, mwenyezi Mungu atawaadhibu watakaoshiriki wizi wa kura kwenye Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020.
Huu ndio ujinga, mbona hakuwaadhibu 2015! Haya mambo ya ujinga wa tunamuachia Mungu hatufiki popote!
 
Sawa.
Lakini this time ccm wasitegemee tutamtaja Mungu tu........Mungu atatajwa huku tunakuja na NYENZO.

Watatutambua mwaka huu.
 
Mungu hapana hapa tutapigana wenyewe huyo mungu miaka yote yupo wapi 2015 hakuwepo
Hapa tukipambana bila uoga hawa ngedere wa CCM mapema tu wanaondoka
 
Back
Top Bottom