LGE2024 ACT Wazalendo: Waungeni mkono vijana uchaguzi wa Serikali za Mitaa

LGE2024 ACT Wazalendo: Waungeni mkono vijana uchaguzi wa Serikali za Mitaa

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Papaa Mobimba

JF-Expert Member
Joined
Jan 27, 2018
Posts
882
Reaction score
3,337
Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo ndugu Ado Shaibu ameendelea na kampeni za uchaguzi wa Serikali za Mitaa, na Novemba 21, 2024 alikuwa Jimbo la Mbeya Mjini, Kata ya Ruanda Mtaa wa Makunguru ambapo amepita mtaa kwa mtaa kuwanadi wagombea.

Ameeleza kuwa chama cha ACT Wazalendo kimelenga kuboresha miundombinu ya barabara kwa kutumia viongozi wake wa mitaa ikiwa watapewa ridhaa katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 27, 2024

Amesema ni muhimu kuwa na msingi imara wa viongozi kuanzia ngazi ya chini ambao watasimamia masilahi ya wafanyabiashara wadogo kwa kuwawezesha kupata mikopo, na mazingira mengine mazuri ya biashara.

 
Back
Top Bottom