Wakati aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo, Juma Duni Haji (Babu Duni) akiagwa leo, chama hicho kinaanza utekelezaji wa sera ya ya kuwaenzi viongozi wake wastaafu.
Babu Duni ameachia ngazi mapema mwaka huu na nafasi yake kuchukuliwa na Othman Masoud ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar.
Sera hiyo inaeleza namna ya kuwaenzi viongozi wa chama hicho waliokitumia kwa heshima, bidii na uaminifu.
Viongozi wanaohusika na sera hiyo moja kwa moja ni kiongozi wa chama mstaafu na mwenyekiti wa chama mstaafu.
Kwa sasa watakaonufaika na sera hiyo ni Juma Duni Haji (mwenyekiti wa chama mstaafu) na Zitto Kabwe (kiongozi wa chama mstaafu).
“Kwa kutambua mchango wao mkubwa katika ujenzi na ustawi wa chama, sera hii inaweka mazingira ya kuhakikisha kuwa viongozi wastaafu wanaendelea kutambulika na kuheshimika na chama na jamii,” inasema sehemu ya sera hiyo.
Hata hivyo, ili viongozi hao wanufaike na sera hiyo lazima wasiwe wamekihama chama au kufukuzwa chama, wakitumikie chama kwa heshima na utii.
Pia, kamati ya uongozi Taifa itakuwa na dhamana ya kuamua iwapo kiongozi husika alikitumikia chama kwa heshima na utii.