LGE2024 ACT Wazalendo yafungua Mashauri 51 ya kupinga Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

LGE2024 ACT Wazalendo yafungua Mashauri 51 ya kupinga Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Mtoa Taarifa

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2024
Posts
213
Reaction score
671
Chama cha ACT-Wazalendo kimefungua mashauri ya uchaguzi 51 ya kupinga matokeo na mwenendo wa uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji uliofanyika Novemba 27, 2024 na kusimamiwa na Ofisi ya Rais-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi).

Kesi hizo zimefunguliwa katika mahakama za wilaya mbalimbali Tanzania Bara na tayari zimeshaanza hatua za awali ambazo ni kutolewa wito wa mahakama kuwaita wahusika (wajibu mashauri) kwa ajili ya kutajwa na kujibu mashauri.

Taarifa ya Mwanasheria Mkuu wa ACT Wazalendo, Omar Said Shaaban iliyotolewa leo Jumatatu, Januari 6, 2025 imezitaja wilaya ambazo mashauri hayo yamefunguliwa kuwa ni Temeke, Lindi, Ilala, Momba, Mkuranga, Mafia, Kigoma, Tunduru, Tandahimba, Kilwa na Kibiti.

“Hatua ya kufungua mashauri haya ni muendelezo wa dhamira ya chama chetu ya kupigania demokrasia na haki za wananchi zililizoporwa wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa,” amesema Shaaban.

1736166181650.png

1736166188206.png
 
Wanapoteza muda na fedha, uchaguzi ulikuwa huru na wa haki
 
Back
Top Bottom