Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
Chama cha ACT Wazalendo kimesema kipo tayari kuunganisha nguvu na vyama vingine vya siasa pamoja na taasisi mbalimbali ili kuhakikisha vinapambania uwepo wa uchaguzi huru na haki mwaka huu.
Akizungumza leo Februari 23 kwenye Kikao cha Halmashauri Kuu ya chama hicho Kiongozi wa ACT Wazalendo Dorothy Semu amesema “Tukielekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2025, ni muhimu kutambua kwamba kuna hujuma na hila zinazotumiwa ili kukata tamaa wananchi.
Soma Pia: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Hali hii inatufanya tuwe na jukumu kubwa la kusukuma ajenda ya kuunda jukwaa la mapambano ya pamoja na vyama makini.”
Semu ameeleza kuwa umoja na vyama vingine ndiyo njia pekee ya kusaidia kuhakikisha upatikanaji wa haki kuelekea uchaguzi na kuzuia njia zote za hujuma dhidi ya vyama vya upinzani.
“Tunahitaji kufanya shughuli za pamoja ili kuimarisha umoja wetu wenye nguvu utakaoleta tija ya mabadiliko. Tunahitaji kupambania kuurejesha uchaguzi. Nchi yetu hasa hakuna uchaguzi. Tutaunganisha nguvu na vyama vyote makini na wadau wa demokrasia nchini.”