Rahma Salum
Member
- Sep 7, 2020
- 30
- 59
Akizungumza katika mkutano na Waandishi wa Habari, Mwanasheria Mkuu wa ACT-Wazalendo, Omar Said Shaaban ameeleza kuwa chama chao hakijaridhishwa na majibu yaliyotolewa na ZEC kufuatia barua waliyoandika Agosti 13.
ACT Wazalendo imeonesha kutoridhishwa na utaratibu uliowekwa na ZEC juu ya kura ya mapema, hivyo kuitaka Tume kutoa ufafanuzi juu ya utaratibu wa kulinda usiri wa kura hizo.
Vilevile, ACT Wazalendo inaitaka ZEC kuweka wazi ikiwa mawakala wa vyama na Wagombea wataruhusiwa kuwepo usiku wa kuamkia tarehe 28 Oktoba, 2020.
Aidha, kufuatia kauli ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi aliyonukuliwa akisema wanatarajia kuwepo kwa wapiga kura ya mapema 7,000, ACT Wazalrndo wanaitaka ZEC itoe ufafanuzi ni vipi wameijua idadi hiyo ikiwa kwa mujibu wa Tume mwisho wa kupeleka maombi ni Oktoba 15.
Kifungu cha 82 cha Sheria ya Uchaguzi ya 2018 kinaeleza kuwa Tume itaweka utaratibu wa kura ya mapema ambao utayafanyika siku moja kabla ya tarehe ya Uchaguzi au siku nyingine yoyote kama itakavyoamuliwa na Tume. Zoezi hilo linatarajiwa kufanyika Zanzibar Oktoba 27 na litahusisha makundi yote ya watendaji wa usimamizi wa Uchaguzi Mkuu.