ACT yaitaka serikali kuimarisha utoaji wa mikopo kwa walemavu

ACT yaitaka serikali kuimarisha utoaji wa mikopo kwa walemavu

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Chama cha ACT Wazalendo kimeitaka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kuhakikisha kuwa utoaji wa mikopo kwa wananchi unazingatia makundi yote, hususan watu wenye ulemavu, bila ubaguzi.

Kauli hiyo imetolewa siku ya Alhamisi na Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Ado Shaibu, wakati wa hafla iliyofanyika nje ya Makao Makuu ya chama hicho, Magomeni, Jijini Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yatakayofanyika tarehe 08 Machi 2025.

Katika hafla hiyo, shughuli mbalimbali zilifanyika, ikiwa ni pamoja na uchangiaji wa damu, maonesho ya ujasiriamali, na huduma za upimaji wa afya, ikiwemo saratani ya shingo ya kizazi na matiti.

Ado Shaibu amepongeza hatua ya Ngome ya Wanawake ya ACT Wazalendo kwa kuandaa zoezi la uchangiaji wa damu, akieleza kuwa mahitaji ya damu nchini bado ni makubwa kutokana na ajali na changamoto za kiafya.

 
Back
Top Bottom