Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Chuo Kikuu Tumaini kimepandisha ada kutoka 1,500,000/= hadi 2,500,000/=.Hii haitakuwa pigo kwa walalahoi? na nini maana kwa Serikali kuondoa kodi kwa taasisi za dini?
Si vyuoni tu, mbona kuna sekondari ambazo ada yake ni kubwa kuliko ya baadhi ya vyuo? hilo nalo liangaliwe
Sawa kabisa,lakini kweli wahusika huwa wanasoma malalamiko na ushauri wa JF?Hicho pekee sio kigezo cha kutumiwa kuongeza ada. Kama ambavyo ada kwenye baadhi ya kindergartens imezidi gharama ya kwenye vyuo - kwa mtazamo wako, una maana ya kusema kwamba kwa kuwa ada ya chuo ni 2.5 million kwa mwaka, basi gharama za kindergaten nazo zisizidi 1 million? Ndicho unachotaka kutuambia au sivyo?
Tunahoji vigezo vilivyotumika kuongeza ada kwa 60%, kitu ambacho kwa mujibu wa muandishi hapo juu, mkuu wa KKKT ameshindwa kikiweka bayana.
Imagine mwanafunzi anaingia mwaka wa pili, mzazi wake amefunga mkanda kumpeleka mwanae hapo; ghafla linatokea ongezeko la asilimia 60 kwenye fees. Amwachishe chuo?