Hicho pekee sio kigezo cha kutumiwa kuongeza ada. Kama ambavyo ada kwenye baadhi ya kindergartens imezidi gharama ya kwenye vyuo - kwa mtazamo wako, una maana ya kusema kwamba kwa kuwa ada ya chuo ni 2.5 million kwa mwaka, basi gharama za kindergaten nazo zisizidi 1 million? Ndicho unachotaka kutuambia au sivyo?
Tunahoji vigezo vilivyotumika kuongeza ada kwa 60%, kitu ambacho kwa mujibu wa muandishi hapo juu, mkuu wa KKKT ameshindwa kikiweka bayana.
Imagine mwanafunzi anaingia mwaka wa pili, mzazi wake amefunga mkanda kumpeleka mwanae hapo; ghafla linatokea ongezeko la asilimia 60 kwenye fees. Amwachishe chuo?