Komeo Lachuma
JF-Expert Member
- Oct 31, 2014
- 7,926
- 17,030
Kawaida yetu watanzania ni fitina, chuki, husda na unafiki.
Leo najitia katika sifa hizo. Simba mmeonesha kitu ambacho Yanga tunapaswa pia kuiga. Najua Yanga wenzangu hili litawakera. Acha mi niseme. Sipendi kuwa mnafiki na kwenda kusemea chooni Mfalme ana masikio ya punda.
Yanga tunawekeza sana kwenye propaganda. Sana kwenye vyombo vya habari na wacha-mbuzi. Pia kuna kipindi tunanunua matches. Najua hili hamtalipenda mi napasua jipu. Si tunataka kupona?
Tucheze mpira bila kelele. Tucheze mpira Uwanjani. Sisi tulipo sasa. Simba walishatoka huko. Ndito maana huoni wakipiga sana kelele. Huoni wakisifiwa hata kwenye ujinga. Sisi tunadekezwa na kujidekeza sana.
Sikutegemea Simba wangekuwa na utulivu waliokuwa nao Angola. Tuna la kujifunza. Simba wanapokuwa na mapungufu hukubali wanayo. Sisi hatukubali na wakati mwingine tunamtafuta wa kumwangushia jumba bofu. TFF.
Tumebaki na madeko tu timu yetu inafanya vizuri mechi za ndani sababu timu zetu hizi tunazifahamu, njaa pamoja na marefa wetu.
Tukaze msuli. Simba tunawanoa sisi wenyewe. Sisi tunapambana sana kuifunga Simba. Simba inachukulia mechi yetu kama mechi nyingine yoyote. Ndiyo maana kwao kwa sasa kutufunga au kufungwa nasi si ishu kubwa.
MIMI NIMESEMA. KAMA UTATOKWA NA POVU LITOE TU.
NIMEKAA PALE 👉