Ada ya mtoto kwa dola, hoteli kwa dola, mbona mshahara wangu kwa shilingi?

Ada ya mtoto kwa dola, hoteli kwa dola, mbona mshahara wangu kwa shilingi?

Hekima Ufunuo

JF-Expert Member
Joined
May 28, 2009
Posts
220
Reaction score
11
Ndugu zangu wana JF nisaidieni, nilalamike wapi?

Narudisha watoto wangu shule na mwingine mmoja anaanza shule, kufika tu shuleni naambiwa ada ni dola za kimarekani kadhaaa, nashangaa, anayenihudumia ananiambia lakini unaweza kulipa kwa shilingi ila utabadilisha kwa kiwango cha 1,400/= kwa dola moja, naendelea kushangaaaa.

Naenda hotelini bagamoyo, nimeamua kupunguza uchovu wa pilika za Dar, nafika naambiwa bia dola mbili, chumba dola kadhaa, nashangaa, nauliza kwani hapa ni marekani? naambiwa shilingi haina msimamo. Nashangaaaaa

Napewa safari ya kikazi kwenda Afrika Kusini, najua niko kwa watu na pesa inayoweza kunisaidia ni Dola au Randi. Nikiwa hotelini nataka kulipa nilichotumia kwa dola, mhudumu ananiambia hapana nenda pale badilisha halafu nipe randi. nashangaaaaaaa.

Who is suppose to manage this in our country? Mr Ndulu? Mr Mkullo? au Mh Raisi? Naamini mtanisaidia. Hili jambo linanikera sana na sielewi ni nani sahihi wa kumlalamikia.

Respct.
 
Hii imezidi sana mikoa ya kitalii! tena ni wizi haswaa, chumba cha hoteli ni elfu 40, mhudumu anakwambia dola 40! anafikiri wewe sijui kichaa vile hutaona tofauti!!! Kuna watu hapa hawafanyi kazi zao ipasavyo.
 
Maumivu ni makubwa sana kwetu sisi tunaotaka kuwapa elimu ya maana watoto wetu wakati kipato chetu ni kidogo.
 
hii kucharge ada na fee mbali mbali kwa dola inawapa fedha nyingi sana wafanya biashara...
mfano nikiwa Arusha wiki iliopita , nilifia hotel Moja inaitwa Corridor Hotel, wakanilipisha dola 120 kwa chumba, kwa kuzingatia exchange rate ya siku ile ambayo ilikua 1365, huu ni wizi. huu ni unyama dhidi ya uchumi.
 
Nguvumali, mimi pia nahisi kuna viongozi wako na maslahi juu ya hili jambo. currency yetu ni shilingi kwanini tulipishwe kwa rate ya dola?
 
ha ha ha.Umenichekesha sana..Ukoloni mambo leo huu..Kila kitu ni kwa dola hata kama hujawahi kuzishika wala hujui kwa kubadilishia wala hata hujui exchange rate yake..Thiis is how we live.
 
Nguvumali, mimi pia nahisi kuna viongozi wako na maslahi juu ya hili jambo. currency yetu ni shilingi kwanini tulipishwe kwa rate ya dola?

upo wizi wa wazi, upo wizi unaopigiwa chapuo na watawala maana wakubwa hawa katika sekta za umma ndio mashare holder katika hotel zao, katika shule hizo na katika taasisi zingine zenye kuendeshwa kiwiziwizi.
wanashindwa kuwachukulia hatua maana wakubwa hawa ndio wanaomiliki ofisi hizo.
kweli ukifanya utafiti utagundua, kuwa wapo waheshimiwa kadhaa.
ila inatuumiza na ni wizi.
 
nyumba, viwanja vinauzwa na kupangishwa kwa dola
bandarini kuna fee unalipa kwa dola
 
Nakumbuka mwanzoni mwa miaka ya 2000 wakati teknolojia ya simu za mkononi inaingia nchini,
gharama ya chini ya airtime voucher ilikuwa ni dola tano.
Tuliibiwa sana.
Ni ufisadi uliokithiri ambao unachangiwa na 'upole' na 'ndio mzee' za watanzania wenyewe.
 
Ndiba usemacho ni kweli, shida iliopo ni kua watu hata kuhoji hawahoji.
chukulia nilipoamua kuhoji kwanini nalipishwa dola, walinijibu watu woote hapa wanalipa dola......... wala sikitu kigeni labda kwako.
 
Hapo ndiyo utajua serikali yetu haiishi kucheza makida, nakumbuka some two or three yrs ago mama Meghji akiwa waziri wa fedha alisema serikali imepiga marufuku kucharge huduma au sales kwa dola lakini wkt huo huo TRA,( idara ya serikali) ilikuwa bado inachaji dola kwa kodi zote za importations. Anywayz hilo agizo vp lilifutwa? au ndio kama kawaida haiwezi kuenforce maagizo yake.
 
Usanii hauwezi kuisha in ths cntry,

sijui labda sifahamu, lakini ukiwauliza wahusika watakuambia, we import zaid than export, so fedha yetu inashuka. Lakini hiyo sio sababu ya kufanya unicharge dola, tena walivyowajanja, wanapandisha pole pole, hadi todate 1,400.

Haina tofauti na mafuta jamani, wanapandisha pole pole, kushtuka BP leo naweka mafuta 1680, its almost 1700 per litre.

Tuna majina tu ya taasisi/Idara nchi hii, ila hawafanyi kazi.
 
Hapo ndiyo utajua serikali yetu haiishi kucheza makida, nakumbuka some two or three yrs ago mama Meghji akiwa waziri wa fedha alisema serikali imepiga marufuku kucharge huduma au sales kwa dola lakini wkt huo huo TRA,( idara ya serikali) ilikuwa bado inachaji dola kwa kodi zote za importations. Anywayz hilo agizo vp lilifutwa? au ndio kama kawaida haiwezi kuenforce maagizo yake.

Nyambala,

Hiyo sheria bado ipo (legal tender is still a Tanzanian Shilling - TZS!). Cha msingi watu kujua ni kwamba, wafanyabiashara wanaweza kuweka bei in any currency provided the TZS equivalent is also provided/declared. Zaidi ya hapo wafanyabiashara kisheria hawatakiwi 'kumlazimisha' mteja kufanya malipo kwa currency tofauti na TZS (i.e. ukitoa/lipa TZS na muuzaji akikataa kupokea anavunja sheria). Hayo yote ni kwa biashara au mauzo yanayofanyika ndani ya Tanzania.
 
hawasimamii kwasababu watendaji wakuu wa sekta za umma ni wamiliki katika biashara kuu zoote hapa nnchini.
Angalia makampuni kuanzia Migodini, viwanda , makampuni makubwa ya mawasiliano, usipomkuta karamagi, utamkuta Lowassa, usipomkuta Mkapa utamkuta Yona, usipomkuta ROSTAM utamkuta GraY Mgonja, usipomkuta Kanali Masawe utamkuta Kipingu......
usipomkuta Mboma utamkuta Dialo.
katika hali hiyo hutegemei ofisa wa kawaida katika ofisi fulani ya umma akawa na uthubutu wa kusimamia sheria wakati zinavunjwa.
ni wizi , ni uhujumu ni utapeli.
 
Nyambala,

Hiyo sheria bado ipo (legal tender is still a Tanzanian Shilling - TZS!). Cha msingi watu kujua ni kwamba, wafanyabiashara wanaweza kuweka bei in any currency provided the TZS equivalent is also provided/declared. Zaidi ya hapo wafanyabiashara kisheria hawatakiwi 'kumlazimisha' mteja kufanya malipo kwa currency tofauti na TZS (i.e. ukitoa/lipa TZS na muuzaji akikataa kupokea anavunja sheria). Hayo yote ni kwa biashara au mauzo yanayofanyika ndani ya Tanzania.
unalipa TzS lililopo wanapiga kwa current exchange rate wakiconvert kutoka dola .
 
Huu ni Ukoloni Mamboleo na wizi. Hebu fikiria mtu anacharge rent kwa dola wakati wewe ni MTZ na dola unaikiaga tu. Tunaipa tu nguvu dola against our Shillingi yetu. Sheria inapindwa hata na serikali yenyewe. Taabu tupu.
 
unalipa TzS lililopo wanapiga kwa current exchange rate wakiconvert kutoka dola .

Kiutaratibu ilitakiwa kama ni bei imebandikwa in USD basi pembeni yake ni lazima kuwe na TZS equivalent ili iwe wazi kwa mteja kabla hajatoa offer yake kwa bidhaa/huduma husika. Kama hulazimishwi kulipa kwa currency tofauti na TZS then sio tatizo la BoT tena.
 
Nyambala,

Hiyo sheria bado ipo (legal tender is still a Tanzanian Shilling - TZS!). Cha msingi watu kujua ni kwamba, wafanyabiashara wanaweza kuweka bei in any currency provided the TZS equivalent is also provided/declared. Zaidi ya hapo wafanyabiashara kisheria hawatakiwi 'kumlazimisha' mteja kufanya malipo kwa currency tofauti na TZS (i.e. ukitoa/lipa TZS na muuzaji akikataa kupokea anavunja sheria). Hayo yote ni kwa biashara au mauzo yanayofanyika ndani ya Tanzania.

Tatizo hapo nadhani si currency unayolipia ila prices ziko rated kwa currency ipi maana unapo rate goods and services kwa forex ina maana bei itaenda ikibadilika kufuatana na thamani ya shillingi vs that forex money that is rated for TShs na hapo ndipo watu wanapoona kuna wizi, for sure iko wazi hapo kua raia wanaoonewa kwani malipo yao (ijara) yako rated in Tshs while consumption iko rated in forex...
 
Okay nakuelewa. Lakini katika msingi huo naona itakuwa vigumu kuwabana kisheria kwa sababu essentially hakuna sheria inayowakataza kubadili bei ya bidhaa au huduma zao. Inakuwa vibaya kwa sababu generally shilling yetu ina depreciate against dollar, otherwise isingalikuwa tatizo! Tatizo kubwa tulilo nalo kama nchi ni kuagiza bidhaa nyingi kutoka nje (hata nyama ya ng'ombe na kuku!). Ili wafanyabiashara wasipate hasara (exchange loss) ni lazima wata peg bei ya bidhaa zao against the currency ambayo walinunulia bidhaa hizo kutoka nje (mostly in USD). Therefore, logically wanachofanya ni correct from the business stand point (not that I'm happy about it)!
 
Back
Top Bottom