Wakuu naombeni msaada kidogo kuhusu haya malipo wanayodai wanasheria pindi unapopeleka nyaraka zako waziidhinishe. Hivi, sheria inasemaje, ni halali kuwalipa kwa kazi hiyo, na kama ni halali ni shilingi ngapi wanatakiwa kulipwa kisheria. Manake kuna wakati nilipeleka fomu zangu mahakamani zisainiwe na kugongwa muhuri, Karani wa mahakama akanipokea na kuniambia nmpe Shilingi 15, kwa kuwa ada ya kira muhuri ni shilingi 5,000. Nilikuwa nahitaji mitatu. Nilipomuomba risiti, akaniambia hiyo mihuri yenyewe ndio risiti tayari, inajitosheleza. Nikashindwa kumbana zaidi. Msaada tafadhali