The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,186
- 4,940
Serikali inapendekeza marekebisho ya Kodi na Ada za Pikipiki (Bodaboda) 2026/2027. Serikali imeamua kutowaingiza wafanyabiashara wa pikipiki (bodaboda) kwenye mfumo wa kodi ya makadirio (presumptive tax), kutokana na ugumu wa utekelezaji wake kwenye sekta hiyo.
Badala ya kodi hiyo, Serikali inapendekeza kufanya marekebisho ya sheria ili kuongeza ada ya usajili wa pikipiki (wa mara moja tu) kutoka Shilingi 95,000 hadi Shilingi 150,000.
Hatua inaelezwa kulenga kulinda biashara hizo ndogo zisiumizwe na kodi za kila mara, huku ikitarajiwa kuingizia Serikali mapato ya ziada ya kiasi cha Shilingi bilioni 17.75.
Wamepunguza Kwa wanamitandao huko wameongeza kwenye pikipiki yani ni kama panya ameamua kuuma kende la kushoto baada yakumaliza kuuma la kulia..badala wapunguze ila ndo wameongeza
Kwa mama, anaupiga mwingi kwakweli.Pongezi kwa nani 😂
hii inaitwa kamua mama kamua,kamua mama usitumie hiriziSerikali inapendekeza marekebisho ya Kodi na Ada za Pikipiki (Bodaboda) 2026/2027. Serikali imeamua kutowaingiza wafanyabiashara wa pikipiki (bodaboda) kwenye mfumo wa kodi ya makadirio (presumptive tax), kutokana na ugumu wa utekelezaji wake kwenye sekta hiyo.