Adamu: Mwanadamu wa Kwanza Ulimwenguni

Adamu: Mwanadamu wa Kwanza Ulimwenguni

John Magongwe

Member
Joined
Jan 4, 2024
Posts
71
Reaction score
119
Adamu: Mwanadamu wa Kwanza Ulimwenguni

Adamu ndiye mwanadamu wa kwanza kuishi ulimwenguni.

Kuumbwa kwa Adamu

“Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai’’ (Mwanzo 1: 26-27; 2:7)
Binadamu wa kwanza ulimwenguni, Adamu na mkewe Hawa. Wote wawili waliumbwa kwa wakati na muda unaofanana katika ulimwengu wa roho (Mwanzo 1:27, 1Wakorintho 15:45). Kwa mujibu wa biblia, alipoumbwa mwanaume ndipo mwanamke naye akaumbwa. Lakini katika ulimwengu wa mwili tunaona Adamu alitolewa kwanza, kisha Hawa alifuata (Mwanzo 2: 21-22).

Adamu alikuja ulimwenguni akiwa mtu mzima, mwanamume kamili. Yaani, kila kitu kinafanya kazi kama mwanaume mwenye akili na mwenye kuweza kuchukua majukumu yake papo hapo alipoletwa ulimwenguni. Hawa naye ni vivyo hivyo.

Hii ni tofauti na ujio wa wanadamu wengine wote, kwa maana sisi wanadamu wengine tuliokuja baadaye ni lazima tuzaliwe katika hali ya uchanga, kisha ndipo taratibu tunaanza kukua, hadi kufikia utu uzima. Lakini pia, Adamu hakuzaliwa na mwanamke ye yote, bali aliumbwa moja kwa moja. Sisi wote tukija duniani ni lazima tuzaliwe na mwanamke. Adamu alipoumbwa tu, alikuwa na uwezo wa mara moja wa kumtambua Mungu aliyemuumba na aliweza kumsikia na kuongea naye.

Adamu hakuhitaji afundishwe kumjua Mungu, wala kumsikia kama leo tunavyopata shida ya kujifunza namna ya kumjua na kumsikia Mungu. Adamu alipozaliwa kwa kuumbwa, kila kitu kilikuwa tayari kinamsubiri yeye kama mtawala. Ni sawa na kusema ulimwengu na unono wake ulikuwa tayari unamsubiri mtawala.

Adamu alipoletwa duniani, katika dakika ile ile, hakulia kama watoto wachanga leo wakizaliwa ni lazima walie. Na endapo kama mtoto aliyezaliwa halii, basi wakunga watatafuta njia mbadala ya kumfanya mtoto/kichanga kilie, ndipo mambo mengine yaendelee, maana kisipolia ni hatari anaweza akawa bubu au kukosa akili timamu, n.k.. Lakini Adamu hakulia na bado akili zake zilikuwa nyingi kiasi kwamba hazikuweza kupimika. Dunia inawaka moto kwa maovu. Kichanga kikiacha enzi yake kutoka huko tumboni kwenye ulimwengu usiokuwa na uharibifu, siku hiyo kikija duniani kwenye ulimwengu wa uovu na dhambi, hapo kitoto lazima kipige kelele na kulia.

Adamu Kuletewa Mke na Mungu

Adamu aliletewa mke anayefanana naye, kwani haikuwa vema yeye kuwa peke yake (Mwanzo 2:18). Mkewe Hawa, alitoka kwa Bwana moja kwa moja. Kwa sababu hiyo, Adamu hakutumia nguvu binafsi kumtafuta mkewe, bali nguvu iliyotumika ilikuwa ni nguvu ya Mungu. Hapa tunapata fundisho kuwa kumbe mke/mume anapaswa aletwe na Mungu mwenyewe. Akili na nguvu zako binafsi hazihitajiki katika kutafuta mwenza wako.

Ingawa biblia haisemi Hawa mwanamke alifinyangwa baada ya muda gani tangu Adamu alipofinyangwa, lakini siku ile Hawa mwanamke alipoumbwa kwa jinsi ya mwili, siku hiyo hiyo Mungu aliwaunganisha/alifungisha ndoa, kati ya Adamu na Hawa. Yaani Adamu alioa siku hiyo hiyo wakawa mume na mke. Mungu mwenyewe aliwafungisha ndoa. Kumbe ndoa halisi ni lazima Mungu mwenyewe ahusike, ndiye awafunge mtu mume na mtu mke na kuwa mwili mmoja. Hii ni kwa sababu ndoa ni wazo la Mungu mwenyewe.

Ndoa ya Adamu na Hawa ndiyo ndoa ya kwanza kabisa ulimwenguni. Ndoa hii ilikuwa ni ya mume mmoja na mke mmoja. Hapa pia tunapata fundisho kuwa, kumbe tangu mwanzo, ndoa ni ya mume mmoja na mke mmoja (Marko 10:6)

Kazi za Adamu

Bwana Mungu akamtwaa huyo mtu, akamweka katika bustani ya Edeni, ailime na kuitunza (Mwanzo 2: 8, 10, 15).
Kuitunza na kuilima bustani (Mwanzo 2:15)
Kabla ya Adamu hajaletewa mke/hajaoa, alikuwa na kazi aliyopewa pale kwenye bustani. Kwa Adamu kupewa kazi bustanini kunaonesha kuwa Mungu ni wa kufanya kazi (Yoh 5:17). Lakini pia, inaonesha kuwa wazo la kufanya kazi ni la Mungu Baba mwenyewe, kwa sababu Mungu ndiye aliyemwuumba Adamu na kukabidhi afanye kazi. Kwa uweza wake Mungu angeliweza kumwacha Adamu akae na kula bila kufanya kazi, kwa sababu katika bustani ya Edeni kulikuwa na kila aina ya chakula, lakini pamoja na uwepo wa chakula kizuri cha kutosha, bado Mungu anampa Adamu kazi za kufanya.

Biblia inatuonesha wajibu wa kwanza aliokabidhiwa Adamu wakati ule kabla ya mwanamke kuumbwa kwa jinsi ya mwili, Adamu alikabidhiwa bustani ailime na kuitunza. Jukumu hili lilikuwa ni kubwa. Lakini Adamu alifanikiwa kuitunza vyema bustani ya Mungu. Hatujui bustani ya Edeni ilikuwa na ukubwa gani, lakini bila shaka eneo lilikuwa ni kubwa, hivyo Adamu alikuwa na kazi nyingi bustanini.

Wajibu wa Adamu kuitunza bustani inatueleza kwamba mwanadamu wa kwanza alikuwa mkulima. Lakini pia, kwenye bustani ile kulikuwa na wanyama. Hivyo, kazi ya kwanza ya mwanadamu ilikuwa ni kulima na kufuga, pasipo na nyezo bora za kisasa na utaalam wa kusomea darasani. Adamu alikuwa na nyenzo halisi za kuifanya bustani iwe hai wakati wote na mifugo ikue na kuongezeka.

Adamu hakwenda kusomea chuo cha kilimo na ufugaji, bali Mungu mwenyewe ndiye alikuwa chuo na elimu katika kazi yote. Mungu alikuwa Baba kwake, alimtegemea katika maarifa. Kumbe kupitia Adamu, tunaweza kujifunza hapo kwamba ikiwa utamtegemea na kumwamini Bwana Mungu, japokuwa hujasoma, lakini Mungu atakusomesha katika darasa lake maalum na Roho mtakatifu atakuchukua hatua kwa hatua.

Kushika agizo la Mungu (Mwanzo 2:15-17)

Adamu ndiye aliyekabidhiwa agizo la kutokula matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya. Kwa kuwa Bwana Mungu ni Mungu wa utaratibu, alijua Adamu ni kiongozi wa nyumba, hivyo kiongozi akabidhiwe agizo na ahakikishe analisimamia katika nyumba yake.

Agizo hilo kwa Adamu lilikuwa ni jepesi na linawezekana kutimizwa kabisa, kwa sababu Mungu asingeweza kumpa Adamu kitu ambacho Adamu hakiwezi. Hata leo, yale anayotuagiza kwa neno lake, yote yapo ndani ya uwezo wetu, ikiwa tupo pamoja naye. Kile ambacho Mungu alichokuwa akikitafuta kwa Adamu ni UTII. Kwa mara ya kwanza Mungu anatoa amri kwa mwanadamu, Adamu. Kulishika agizo/amri ilikuwa ni wajibu wa Adamu muhimu kuliko vyote. Kwa sababu wajibu huo ulishikilia msingi wa maisha yake yote.

Ibada (Mwanzo 3:8-9)

Kuzungumza na Mungu ni ibada. Kupitia Mwanzo 3:8-9, tunaona kumbe ilikuwa ni utaratibu wa Mungu kushuka na kuzungumza na Adamu pamoja na Hawa. Hata kabla ya Hawa kuumbwa kulikuwa na muda mzuri wa Adamu kujiwasilisha kwa Mungu. Hii ilikuwa ni ibada ya moja kwa moja. Adamu alijua namna impasavyo ya kumwabudu Bwana Mungu wake. Kwa kuwa Adamu alikuwa rohoni kabla ya anguko, hivyo Roho wa Mungu alimwongoza yote yampasayo kufanya. Tunaposema Roho mtakatifu ni mwalimu hakika tunamaanisha. Yeye ni mwalimu (Yoh 14:26). Ibada ilikuwa jambo la muhimu kama wajibu ambao Adamu aliacha vyote na kukaa na Bwana katika mazungumzo.

Hapakuwa na mchungaji na washirika wengine kwa jinsi ya mwili kama ilivyo leo, lakini malaika waliopo zamu walimwatamia Adamu wakati wote. Hata wakati ule wa ibada, uwepo wa Mungu ulijaza nafasi ya washirika. Viumbe vingine vilivyoumbwa na Bwana vilikuwa sehemu ya ibada.

Huyo ndiye alikuwa Adamu, mwanadamu wa kwanza ulimwenguni, kutoka kuumbwa kwake, kuletewa mke na Mungu, hadi kuishi na kufanya kazi kwenye bustani ya Edeni. Baadaye, Adamu aliishi nje ya bustani ya Edeni.

Siku zote za Adamu alizoishi ni miaka mia kenda na thelathini, naye akafa (Mwanzo 5:5). Hivyo Adamu aliishi miaka 930.

Adamu, hakuwa mtu aliyeishi miaka mingi kuliko wote. Maandiko yanarekodi kuwa, siku zote za Methusela ni miaka mia kenda na sitini na kenda, akafa (Mwanzo 5:27). Methusela ndiye mwanadamu aliyeishi miaka mingi zaidi ulimwenguni, miaka 969.
 
Thibitisha.
 
Ukiangalia historia kwa mwelekeo wa Bible, Adamu ameishi hapa duniani miaka 6000+ iliyopita, lakini tukija kwenye shahidi za kisayansi, kuna mabaki ya binadamu yaliyogunduliwa yenye umri mkubwa zaidi ya Adamu, sasa tunathibitisha vipi kama Adamu ndiye mwanadamu wa kwanza kuumbwa na Mungu?.

cc

Adam alizaliwa na miaka mingapi
 
Ukiangalia historia kwa mwelekeo wa Bible, Adamu ameishi hapa duniani miaka 6000+ iliyopita, lakini tukija kwenye shahidi za kisayansi, kuna mabaki ya binadamu yaliyogunduliwa yenye umri mkubwa zaidi ya Adamu, sasa tunathibitisha vipi kama Adamu ndiye mwanadamu wa kwanza kuumbwa na Mungu?.

cc
John Magongwe
Ni uzushi tu, hakuna cha adam wa nini.
 
Back
Top Bottom