Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
"Kama Mbwai na Iwe Mbwai." Ndiyo kauli anayoitumia Mwenyekiti wa Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC) taifa, Shaban Itutu akielezea msimamo wa chama hicho kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.
Itutu ametoa kauli hiyo, baada ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu kuzungumza katika majukwaa mbalimbali akieleza kwamba 'No Reform, No Election' akimaanisha kwamba iwapo hakuna mabadiliko hakuna uchaguzi wa mwaka huu.
Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Hata hivyo, akizungumza jana (Ijumaa) alipotembelea Ofisi za Mwananchi Communications Limited (MCL) zilizopo Tabata Relini Dar es Salaam, Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Amos Makalla asisitiza kuwa uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu utafanyika kama ilivyopangwa na kuwataka wananchi wasidanganywe na kauli za "No Reform, No Election".
Akizungumza leo Jumamosi Februari 22,2025, alipondua Tawi la ADC Kata ya Nyamanoro wilayani Ilemela mkoani Mwanza, Itutu amesema chama hicho hakitasusia uchaguzi badala yake kimeamua "Kama Mbwai na Iwe Mbwai" katika uchaguzi ujao.
Kwa upande wake, Mkazi wa Nyamanoro na mwanachama wa chama hicho, Hamisa Estam amesema namna pekee ya kupambana na changamoto hizo ni kuongeza ushawishi kwa wapigakura wajitokeze kwa wingi ili uamuzi ufanyike kwenye 'sanduku la kura.'