Addict wa chai na kahawa

Addict wa chai na kahawa

baghozed

JF-Expert Member
Joined
May 26, 2011
Posts
532
Reaction score
97
naomba ushauri wenu mi ni mnywaji mzuri sana wa chai na kahawa (haswa chai) sasahuwa nikinywa hivyo vinywaji huwa nakojoa sana,sasa hilo laweza kuwa tatizo??na je kuna tatizo lolote laweza nipata kwa kutumia hivyo vinywaji???
Ahsante
 
Kawaida yako unakunywa vikombe vingapi vya chai/kahawa kwa siku?
 
Mimi nkunywa chai 3asubuhi 3 m chana na jiuon havielezeki wacha tu kama ni sumu mie nshakufa na niliamua hivi baada yakuacha masoda haya lol
 
sinywi nikiwa na hamu na hizo soda nakunywa maji kukata kiu nikizidiwa sana naenda kwenye dompo basi



lakini stone tangawizi hazina madhara nivea

usiogope kuinywa kama una hofia ile mikemikali
 
Mkuu,
Pole kwakuwa teja wa kaffeina. Katika chai na kahawa kuna kitu kinaitwa caffeine/kaffeina ambacho ni mojawapo ya madawa ya kulevya kundi la stimulants/madawa yanayokusimua, kukuamsha na kukupa Hi. Kaffeina pia huambatanishwa katika dawa na vidonge mbalimbali za kutuliza maumivu mwilini.

Hivyo chai au kahawa ni MADWA YA KULEVYA PIA. Hii ndiyo sababu wale waliozoea kunywa chai kila siku siku wasipokunywa hujisikia kichwa kuuma.

Kaffeina hupatikana katika chai ya rangi, kahawa na karibu katika soda za juisi zote za viwandani. Kuna pombe inaitwa wanzuki kama sikosei hutengenezwa kwa kutumia: maji+sukari+majani ya chai, hivyo kinachoifanya iitwe pombe na watu walewe ni hayo majani ya chai, na watu wanaotumia pia huwa vigumu kwao kuiacha.

Kama wewe ni mpenzi wa chai au ile hali ya maji ya moto asubuhi, nakushauri badala ya kutumia majani ya chai meusi ni bora uwe unatumia tangawizi, mdalasini, mchaichai, chai masala au hata ndimu pekee.

Chai ya rangi au kahawa husababisha matatizo lukuki katika miili yetu kuanzia kupungukiwa kumbukumbu mpaka kansa. Soma maelezo kuhusu kaffeina inavyohusishwa na kansa katika link ifuatayo:

Kansa/Saratani | maajabuyamaji.net
 
duh, kumbe naweza kuwa hatarini pia?
Sasa ninywe nini, vingine vyote situmii tena, yaani ninywe maji tu?
 
Siku hizi kuna majani ya chai yasiyo na caffein yanaitwa Green tea, pia kuna roibos, hibscus yanapatikana supermarkets. Lakini pia hatari nyingine ya ulevi wa chai/kahawa ni kiasi cha sukari unachotumia kwa siku nzima. Waweza kuona uko fit sasa lakini fainali uzeeni. Punguza kiasi cha sukari per cup au tumia asali
 
acheni zengwe lenu bana, kwa ninyi kila kitu kinaweza kuwa sumu. hata kuishi duniani tu ni sumu. ndiyo maana mungu akatuumba na maini na mafigo na mapafu na ngozi. kazi ya organi zote hizo nilizozitaja nia kuchuja hizo sumu mnazozisema na kuzitoa nje ya mwili kama taka mwili ikiwa ni pamoja na mkojo, jasho na hewa tunayopumua nje. so kama ingekuwa dunia kwa asili ni salama Mungu asingeweka hizo organ bana. so natural poison (sumu za asili - ndo kama hizo caffein kwenye chai au kahawa, amonia kwenye nyama, n.k) are not harmful to the body, unless organ zako zime fail. ndo maana ini au figo zikifail huwezi ishi zaidi ya saa 24
 
Hii ya cancer kutokana na chai mmh kumbe niko kwenye deathrow longtime
 
Haya maisha kila kitu sumu, sijui tutapataje kupona..Lol
 
acheni zengwe lenu bana, kwa ninyi kila kitu kinaweza kuwa sumu. hata kuishi duniani tu ni sumu. ndiyo maana mungu akatuumba na maini na mafigo na mapafu na ngozi. kazi ya organi zote hizo nilizozitaja nia kuchuja hizo sumu mnazozisema na kuzitoa nje ya mwili kama taka mwili ikiwa ni pamoja na mkojo, jasho na hewa tunayopumua nje. so kama ingekuwa dunia kwa asili ni salama Mungu asingeweka hizo organ bana. so natural poison (sumu za asili - ndo kama hizo caffein kwenye chai au kahawa, amonia kwenye nyama, n.k) are not harmful to the body, unless organ zako zime fail. ndo maana ini au figo zikifail huwezi ishi zaidi ya saa 24

Nikweli mkuu, lakini kumbuka hizo ogani zingekuwa zinafanya kazi bila shida kama unavyosema wewe Basi tusingekuwa tunasikia kuna hospitali au zahanati au kituo fulani wanatoa huduma za kutoa au kufyonza sumu mwilini, si ini, ngozi na mapafu vinafanya kazi kama unavyosema?.

Ni kweli ogani hizo hufanya kazi hiyo lakini kwa sababu we unaendelea kuongeza masumu daily katika vyakula vinywaji vyako, nazo hufika wakati huchoka ama huzidiwa. Na kama ni hivyo hizo ogani zinatosha kwa kazi hii kwanini wameandika katika pakiti za sigara kuwa uvutaji wa sigara ni hatari kwa afya yako? au kama siku hizi tunavyosikia kuhusu pombe kuwa kunywa pombe kupita kiasi ni hatari kwa afya yako and that you need to drink responsibly?.

Hata hivyo signature yako inatosha kutupa jibu la unayobisha hapa.
 
Hii ya cancer kutokana na chai mmh kumbe niko kwenye deathrow longtime

Kwa kawaida kansa huishi katika mazingira ya asidi pekee na tunajuwa kuwa chai na kahawa vimejaa asidi too much asidi, pia tunajuwa kuwa kansa haiji mwilini kwa siku moja! ni matokeo ya muda mrefu ya kutotumia vyakula, kemikali na vinywaji visivyo sahihi kwa muda mrefu.
 
Haya maisha kila kitu sumu, sijui tutapataje kupona..Lol

Siyo kila kitu ni sumu mkuu, unapaswa kusoma katika vibandiko vya kila bidhaa unayotumia iwe ni soda, juice, mafuta unayopaka mwilini, chakula unachokula nk kujuwa vimetengenezwa kutokana na nini na hivyo vitu vilivyotumika kutengeneza bidhaa hiyo vina faida chanya ngapi na faida hasi ngapi na mhimu kuliko yote ni je mwili wako unauona unavihitaji hivyo unavyotumia? kwa faida gani?.

We unaona mama anakaanga samaki katika mafuta machafu na meusi tii tena kila siku bila kuyamwaga wala kuyabadilisha kisha wewe unaenda kununua hizo samaki halafu unabaki kulalamika kila kitu ni sumu. Kielewe kwanza.
 
duh, kumbe naweza kuwa hatarini pia?
Sasa ninywe nini, vingine vyote situmii tena, yaani ninywe maji tu?

Kunywa chai mkuu, unachotakiwa kufanya ni kutotumia hayo majani ya chai meusi, badala ya hayo majani meusi unaweza kutumia tangawizi, mdalasini, tea masala (mchanganyiko wa viungo/spices mbalimbali), unaweza pia kukamulia ndimu tu katika maji yako ya moto na kuongeza sukari inatosha. Unaweza pia kujinunulia blenda na ukajitengenezea mwenyewe juisi nyumbani kwako kwa kutumia matunda yetu ya kawaida.
 
Back
Top Bottom