Aden Rage: Ni muda muafaka wa TFF kuungana na ZFA kuunda chombo kimoja cha Kuwaongoza

sembo

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
4,350
Reaction score
3,451
Kama njia ya kuondoa malalamiko ya chama cha soka Zanzibar [ZFA] kua soka la Zenji linahujumiwa na TFF.. Aden Rage amependekeza leo Bungeni kuundwa kwa chombo kimoja kitakachosimamia kabumbu nchini Tanzania, tofauti na sasa ambapo kuna TFF na ZFA. Ametolea mfano wa Shirikisho La Olimpiki Tanzania [TOC] ambalo huoperate Tanganyika na Zanzibar..

Akijibu swali hilo Naibu Waziri wa michezo, Juma Nkamia alidai kua watakaa Serikali, TFF, ZFA na wadau wengine kuona wanalishughulikia vipi hilo suala.

Maoni Yangu.

Naungana na Rage kwani;

1. Yale malalamiko ya ZFA kua inabaniwa kujiunga FIFA na TFF yataisha.

2. Tutafaidika zaidi na vipaji vingi toka Zanzibar katka ligi kuu itakayojumuisha timu za Zenji.. Tutegemee kuwaona kina Nadir, Babi n.k wengine.

3. Yale madolari yanayotolewa na FIFA kila mwaka, yatatumika pia kuendeleza soka la zenji.. tofauti na hali ilivyo sasa.
 
Wakati ZFA wanatafuta uanachama FIFA mtu anasema waungane na TFF. Kesho yataanza malalamiko ya kumezwa na bara.

Waendelee kupigania uanachana FIFA, huenda kilio chao kikasikika!
 
Tuaache wazanzibar wajitafutie uwanachama FIFA huenda wanaweza kufanya vizuri katika mashindano mbalimbali yanayotambuliwa na FIFA.
 
Wakati ZFA wanatafuta uanachama FIFA mtu anasema waungane na TFF. Keshio yataanza malalamiko na kumezwa tena.

Waendelee kupigania uanachana FIFA, huenda kilio chao kikasikika!

Ni rahisi kwa Tanzania kuwa na serikali moja ya muungano kuliko kuwa na chama kimoja cha soka.
 
Ni rahisi kwa Tanzania kuwa na serikali moja ya muungano kuliko kuwa na chama kimoja cha soka.

Huo muungano wa TFF na ZFA utaleta kelele nyingi sana. Mwisho utaambiwa Taifa Stars nusu watoke Zanzibar bila kujali ubora wa mchezaji. Wala siafiki ligi ya muungano.
 
Huo muungano wa TFF na ZFA utaleta kelele nyingi sana. Mwisho utaambiwa Taifa Stars nusu watoke Zanzibar bila kujali ubora wa mchezaji. Wala siafiki ligi ya muungano.

Rage amechemka vibaya sana kupendekeza jambo ambalo anajua haliwezekani.
 
Ikumbukwe kua Rage amekua kiongozi wa FAT sasa TFF kwa mda, hivyo anajua in and out mambo yalivyo.. Maoni yake si yakuyapuuza.
 
Tuaache wazanzibar wajitafutie uwanachama FIFA huenda wanaweza kufanya vizuri katika mashindano mbalimbali yanayotambuliwa na FIFA.

Mkuu mkolaj ili kua mwanachama wa FIFA nchi husika LAZIMA iwe mwanachama wa Umoja wa Mataifa.. Hiki ndicho kilichowakwamisha na kitaendelea kuwakwamisha ndugu zetu wa Zenji.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu, huyu mheshimiwa aliisha kuwa katibu mkuu wa FAT. Kwa nini hakuona haja hiyo?
 
Mkuu, huyu mheshimiwa aliisha kuwa katibu mkuu wa FAT. Kwa nini hakuona haja hiyo?

Nadhani alikua akiogopa kuwanyima mabosi wake kina Ndolanga ulaji pia ili kulinda kibarua chake, ndo mana akakaa kimya.. Sasa yupo nje ndo anaamua kueleza maono yake.
 
Sidhani kama ni jambo la busara kuungana na ZFA kwanza huko Zanzibar wanadai hawataki pombe TFF wakipata udhamini wa Serengeti tayari mgogoro utaanza.
 
Mkuu mkolaj ili kua mwanachama wa FIFA nchi husika LAZIMA iwe mwanachama wa Umoja wa Mataifa.. Hiki ndicho kilichowakwamisha na kitaendelea kuwakwamisha ndugu zetu wa Zenji.

Si kweli
Sina data kamili tu hapa karibu, but last time i checked FIFA ilikuwa na wanachama wengi zaidi ya UN
 
Last edited by a moderator:
Si kweli
Sina data kamili tu hapa karibu, but last time i checked FIFA ilikuwa na wanachama wengi zaidi ya UN

Unachosema ni kweli, unaweza kua mwanachama nusu nusu na ukakosa fulsa wanazopata wanachama kamili.. mf. wa mwanachama nusu nusu ni Hong Kong ambao hawapati nafasi ya kushiriki michuano inayoandaliwa na FIFA ingawa wanapata misaada toka FIFA... Sasa uanachama wa aina hii hautawasaidia ndugu zetu wa Zenji.
 
TFF na ZFA zitaungana tu endapo Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzani itatambua Serikali moja, vinginevyo ni kuota ndoto za mchana.

Ila Mkuu kuna Shirkisho La Michuano ya Olimpiki [TOC] ambalo ni miksa ya Tanganyika na Zenji.. Nadhani wakiamua wanaweza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…