Adha za "Kibanda Umiza"

Adha za "Kibanda Umiza"

okaoni

JF-Expert Member
Joined
Jun 25, 2011
Posts
1,471
Reaction score
1,303
Leo nilienda kuiangalia timu yetu ya Taifa ilipokuwa inamenyana na Uganda. Kuna baadhi ya kero nilizokutana nazo naomba niwashirikishe.

1. Watu wanapiga kelele hovyo hovyo kiasi kwamba kuna limtu lenyewe linajifanya ndio lichambuzi mashuhuri ni kukosoa tuu tena kwa sauti kubwa hata yale maneno ya watangazaji huyasikii.

2. Tv zipo chini ukia mfupi unaweza kuishia unaangalia visogo vya waliombele yako badala ya mpira. Mbaya zaidi linakuja limtu lirefu kuliko wote halafu limevaa kofia ndio linakaa mbele yenu, uliliambia hata lifue kofia wengine muone kesi inaanzia hapo.

3. Linakuja lilevi na lenyewe linaanza kupiga kelele huku mdomo ukitema harufu ya matautapu.

4. Kutokana na mbanano ndani ya banda hilo joto linazidi na minjemba inavua mashati.... kikwapa chake sasa!!!!!?

5. Kipindi cha mapumziko banda linakuwa kama treni za zamani za mosho mijamaa inaanza kuwasha sigara kero kweli kweli

6. Nimeshangaa leo baadhi ya watanzania wanashangilia baadhi ya wachezaji wa timu ya uganda na uganda kwa ujumla huku wanaiombea njaa Taifa stars. Nilishangaa na nikakasirika, na kama nilikuwa na mamlaka nilikuwa nawapiga amri ya kupotea nchini ndani ya masaa 49 (persona non granta) waende kwenye nchi waliokuwa wanaishabikia maana nimeona ni wasaliti wa hali ya juu
 
Mkuu kawaida kwenye vibanda umiza kwani ndio mara yako ya kwanza huko?
 
6. Nimeshangaa leo baadhi ya watanzania wanashangilia baadhi ya wachezaji wa timu ya uganda na uganda kwa ujumla huku wanaiombea njaa Taifa stars. Nilishangaa na nikakasirika, i

Wamebet hao mkuu...
 
Pole sana mkuu,
Umetoa malalamiko yako,ni vizuri ila ulitakiwa uje na solution,nini kifanyike?
 
Iko kibanda umiza ni cha mitaa ya wapi mkuu!!
Mbona vya huku kwetu TV zipo juu,hawaruhusu sigara na vingine mabenchi yanakua marefu kadri umbali kutok kwny TV unavyoongezeka
 
Leo nilienda kuiangalia timu yetu ya Taifa ilipokuwa inamenyana na Uganda. Kuna baadhi ya kero nilizokutana nazo naomba niwashirikishe.

1. Watu wanapiga kelele hovyo hovyo kiasi kwamba kuna limtu lenyewe linajifanya ndio lichambuzi mashuhuri ni kukosoa tuu tena kwa sauti kubwa hata yale maneno ya watangazaji huyasikii.

2. Tv zipo chini ukia mfupi unaweza kuishia unaangalia visogo vya waliombele yako badala ya mpira. Mbaya zaidi linakuja limtu lirefu kuliko wote halafu limevaa kofia ndio linakaa mbele yenu, uliliambia hata lifue kofia wengine muone kesi inaanzia hapo.

3. Linakuja lilevi na lenyewe linaanza kupiga kelele huku mdomo ukitema harufu ya matautapu.

4. Kutokana na mbanano ndani ya banda hilo joto linazidi na minjemba inavua mashati.... kikwapa chake sasa!!!!!?

5. Kipindi cha mapumziko banda linakuwa kama treni za zamani za mosho mijamaa inaanza kuwasha sigara kero kweli kweli

6. Nimeshangaa leo baadhi ya watanzania wanashangilia baadhi ya wachezaji wa timu ya uganda na uganda kwa ujumla huku wanaiombea njaa Taifa stars. Nilishangaa na nikakasirika, na kama nilikuwa na mamlaka nilikuwa nawapiga amri ya kupotea nchini ndani ya masaa 49 (persona non granta) waende kwenye nchi waliokuwa wanaishabikia maana nimeona ni wasaliti wa hali ya juu
kuna watu hujifanya hawaipendi timu yao ilhali wanaipenda na wamelipa hela kuitazama
 
Ndio maana vinaitwa 'vibanda umiza' yaani unaangalia ukiwa unaumia
 
Leo nilienda kuiangalia timu yetu ya Taifa ilipokuwa inamenyana na Uganda. Kuna baadhi ya kero nilizokutana nazo naomba niwashirikishe.

1. Watu wanapiga kelele hovyo hovyo kiasi kwamba kuna limtu lenyewe linajifanya ndio lichambuzi mashuhuri ni kukosoa tuu tena kwa sauti kubwa hata yale maneno ya watangazaji huyasikii.

2. Tv zipo chini ukia mfupi unaweza kuishia unaangalia visogo vya waliombele yako badala ya mpira. Mbaya zaidi linakuja limtu lirefu kuliko wote halafu limevaa kofia ndio linakaa mbele yenu, uliliambia hata lifue kofia wengine muone kesi inaanzia hapo.

3. Linakuja lilevi na lenyewe linaanza kupiga kelele huku mdomo ukitema harufu ya matautapu.

4. Kutokana na mbanano ndani ya banda hilo joto linazidi na minjemba inavua mashati.... kikwapa chake sasa!!!!!?

5. Kipindi cha mapumziko banda linakuwa kama treni za zamani za mosho mijamaa inaanza kuwasha sigara kero kweli kweli

6. Nimeshangaa leo baadhi ya watanzania wanashangilia baadhi ya wachezaji wa timu ya uganda na uganda kwa ujumla huku wanaiombea njaa Taifa stars. Nilishangaa na nikakasirika, na kama nilikuwa na mamlaka nilikuwa nawapiga amri ya kupotea nchini ndani ya masaa 49 (persona non granta) waende kwenye nchi waliokuwa wanaishabikia maana nimeona ni wasaliti wa hali ya juu
Welcome on board!
 
Kuna majina ya kupendeza huko kama Chogo -Henry, Nyoshi- Fellaini, Ndanda Kosovo-Bakayoko, Ustaadhi- Salah
 
Nunua TV yako ubaki nyumbani tu Mkuu.. kama utaki hizo ADHA
 
Bosi nilichelewa kwenye mishemishe ndio ikabidi nijichanganya uswahilini huko huko sasa hayo ndio yamenikuta
 
Mkuu vibanda umiza vinafaida kubwa sana kwenye maisha ya kila sku....mtu mwenye biashara fulani akijichanganya hapo wateja wake wakuu huwa wadau wa vibanda umiza
 
Back
Top Bottom