okaoni
JF-Expert Member
- Jun 25, 2011
- 1,471
- 1,303
Leo nilienda kuiangalia timu yetu ya Taifa ilipokuwa inamenyana na Uganda. Kuna baadhi ya kero nilizokutana nazo naomba niwashirikishe.
1. Watu wanapiga kelele hovyo hovyo kiasi kwamba kuna limtu lenyewe linajifanya ndio lichambuzi mashuhuri ni kukosoa tuu tena kwa sauti kubwa hata yale maneno ya watangazaji huyasikii.
2. Tv zipo chini ukia mfupi unaweza kuishia unaangalia visogo vya waliombele yako badala ya mpira. Mbaya zaidi linakuja limtu lirefu kuliko wote halafu limevaa kofia ndio linakaa mbele yenu, uliliambia hata lifue kofia wengine muone kesi inaanzia hapo.
3. Linakuja lilevi na lenyewe linaanza kupiga kelele huku mdomo ukitema harufu ya matautapu.
4. Kutokana na mbanano ndani ya banda hilo joto linazidi na minjemba inavua mashati.... kikwapa chake sasa!!!!!?
5. Kipindi cha mapumziko banda linakuwa kama treni za zamani za mosho mijamaa inaanza kuwasha sigara kero kweli kweli
6. Nimeshangaa leo baadhi ya watanzania wanashangilia baadhi ya wachezaji wa timu ya uganda na uganda kwa ujumla huku wanaiombea njaa Taifa stars. Nilishangaa na nikakasirika, na kama nilikuwa na mamlaka nilikuwa nawapiga amri ya kupotea nchini ndani ya masaa 49 (persona non granta) waende kwenye nchi waliokuwa wanaishabikia maana nimeona ni wasaliti wa hali ya juu