mopaozi
JF-Expert Member
- Nov 17, 2010
- 3,300
- 523
Ujinga umefungwa ndani ya moyo wa mtoto; Lakini fimbo ya adhabu itaufukuzia mbali kama humpendi utamchukia mwanawo; Ila kama unampenda utamrudi mapema
. Usimnyime mtoto wako mapigo; Maana ukimpiga kwa fimbo hatakufa. Utampiga kwa fimbo, na kumwokoa nafsi yake na Kuzimu.
Kuna usemi usemao Mkunje samaki angali mbichi huu ni ukweli, make ukitaka kumkunja samaki mkavu anavunjika, na usemi mwingine unasema Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo.
*Kila kunapokucha kuna ongezeko kubwa la idadi ya watoto na Vijana ambao ni mzigo kwa wazazi na jamii kutokana na tabia zao. Utasikia akina mama wanalalamika wakisema Heri tumbo hili lisingezaa. Kuna watoto na Vijana ambao ni Mizigo isiyobebeka. Lakini hebu tujiulize chanzo chake ni nini? Kwa sehemu kubwa, tatizo ni malezi tangia walipozaliwa.
*
Sasa hivi kuna haki za watoto, nchi zingine ukimpiga mtoto wako unapelekwa mahakamani, hivyo mzazi haruhusiwi kumrudi mtoto anapofanya ujinga, pia kuna sheria hadi mashuleni ya kutowachapa watoto viboko. Lakini hata majumbani wazazi wengi wamewafanya watoto kama mayai, mtoto ni usiniguse, wanadekezwa hadi wanakuwa mazezeta, utakuta mtoto analia lia ovyo bila sababu, anataka chochote wakati wowote, na mzazi anakubaliana naye, huku anaendeshwa kama gari bovu. Watoto wamejaa ujeuri, ni wasumbufu hadi kwenye majumba ya Ibada, wamejaa viburi na ukorofi, ukijaribu kuwakemea usishangae kukutana na TUSI au Kukufyonya huku akitoa jicho ka mjusi aliyebanwa na mlango.
*
Wazazi wengi hawana Muda wa kukaa na kuchunguza tabia za watoto, lakini kibaya zaidi ni pale wanapoona ni Ustaarabu au Maendeleo kutowarudi watoto, HIYO NI HATARI, akina mama wengi utasikia wanasema, Nitamwambia Baba yako akirudi huku baba mwenyewe anarudi majogoo, huo ni udhaifu mkubwa, mama chukua hatua ya kumrudi mtoto akikushinda ndipo utafute msaada. Siku moja nilisikia Binti akisema Nitakunywa Sumu na mama aksema Basi mwanangu nenda usijenifia bure alikuwa anamkataza kwemda kwa Boy Friend wake. Hayo sio malezi, wazazi lazima tuwe na msimamo au laa kesho ni Majuto.
*
TAHADHARI:
Tumia hekima na busra unapoamua kumwadhibu mtoto, usitoe adhabu ukiwa na hasira, usimwadhibu mtoto kwa kila kosa, usimwadhibu mtoto bila ya yeye kulielewa kosa lake. Wazazi wengi ni wakali na wakorofi kwa watoto, hatimaye wamewafanya watoto kuwa Sugu. Ukali na Hasira havisaidii, wengine kosa dogo tu anamrushia stuli, mara Kofi na tusi juu, mara anamtandika na mwiko wa ugali wa moto, au chohote kilicho mbele yake, huo sio ustaarabu, unaharibu watoto. Fimbo ni hatua ya Mwisho baada ya kutumia kila njia ya kumwelimisha na kumuonya. Na umkalishe chini, umwambie kwa nini umeamua kumpa adhabu.