Adhabu kali zilizowahi kutolewa duniani

Adhabu kali zilizowahi kutolewa duniani

Heri lee

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2013
Posts
981
Reaction score
537
(SEHEMU YA KWANZA)

ADHABU MBAYA NA HATARI SANA KUWAHI KUTOLEWA DUNIANI KATIKA UTAWALA WA UAJEMI

Kumekuwepo na adhabu nyingi kutolewa katika hiki kipindi chetu (Dunia ya sasa) ambazo watu wengi wanaona kama ni hatari sana na ni ukiukwaji wa haki za binadamu. Mfano adhabu ya kunyongwa, adhabu ya kuchinjwa ambayo inatumika sana katika nchi za kiarabu kama Saudiarabia kitendo cha kuchinjwa hadharani..

Hizi adhabu zinapingwa vikali na mashirika ya kutetea haki za binadamu, kwa namna moja au nyingine mashirika haya yameweza kupaza sauti na kusikilizwa, kwani kuna nchi duniani tayari zimefuta adhabu hizi za vifo kwa wakosaji.. Ila kiuhalisia hizi adhabu za sasa hakuna kitu kabisa ukiweza fananisha na adhabu za kale kama ambazo tutaenda kuziona Leo kwa hawa waajemi, ni adhabu ambazo hazitakiwa tena kurudishwa katika jamii yetu ya sasa kwani zilikuwa ni za kishetani kabixa, zenye mateso makali na ukiukwaji wa haki za kibinadamu, kwani inafikia unatamani ufe harakaharaka kwa maumivu upatayo.

Wapenzi na wafuasi wa bibilia kama kitabu cha Muumba lakini kama chanzo cha maarifa uliojaa kila kitu, tunajifunza kumewahi kuwepo na tawala kubwa NNE zilizotikisa Dunia ya wakati huo.

1:BABYLON (Iraq ya sasa) - chini ya Mfalme NEBUCHADNEZZAR.
2:UMEDI NA UAJEMI (Wairan wa sasa) - Chini ya KORESHI, ALTASHASTA na wafalme wengine baadae.
3:WAYUNANI (Wagiriki) - Chini ya ALEXANDER MKUU.
4😀OLA LA RUMI (waitaliano) - Chini ya KAISALI.

LEO TUJIKITE NA KUANGALIA ADHABU ZA HAWA WAAJEMI:
HAwa watu waliamini katika Haki. Na walikuwa makini sana katika kutoa adhabu zao ili mtu yoyote asionewe. Ila ukipewa adhabu kwa kosa kubwa ni adhabu hasa na usiombee ukakutana nazo.

Hapa chini ni ADHABU ZENYEWE;

1:KULAZIMISHA WATU KULA WATOTO WAO

Kama umewahi kufanya makosa madogo ya kuchukulia kawaida agizo la mkuu wa nchi, hilo ni huku sio Uajemi ya enzi hizo. Siku moja mfalme aliota ndoto mjukuu wake atampindua kwenye utawala. Akamwagiza Jemedali wake mmoja Aitwae Harpagus amchukue huyo mjukuu na akamtupe afie Porini. Jamaa akajiongeza akamuacha huyo mtoto kwa mchunga kondoo mmoja na kulelewa hapo. Miaka kumi baadae ikajulikana kwa mfalme kuwa jamaa hakutii agizo.

SEHEMU YA PILI)ADHABU MBAYA NA KALI ZAID KUWAHI ZILIZOWAH KUTOLEWA
Mtoto wa Harpagus alichukuliwa akakatwa mkono na kutolewa Koromeo Kisha vikarostiwa vizuri na katika sherehe iliyokuwepo jamaa akawekewa nyama ya mtoto wake. Katikati ya mlo akaulizwa kama anatambua anachokula. Ndipo mwili uliobakia ukaletwa na jamaa akalazimishwa amalizie kuula hadi atakaposhiba. Alijua kosa lake na akaapa kuwa mtiifu na kula huyo mtoto na kuondoka na mabaki yake hadi nyumbani kwake na kumzika.
Adhabu hii kwake ilitekelezwa kwa upendo na heshima nyingi.

2: MMOJA KUUWAWA MARA TATU KWA MPIGO

Waajemi waliamini Kuna baadhi ya watu walistahili kufa zaidi ya mara moja. Ukifa haraka utakuwa umefaidi na hujajifunza. Kiukweli Sio unakufa mara tatu ila unapitia mateso matatu makali sana ambayo ni kama umekufa, kabla ya Pumzi kukata.

Towashi mmoja alipomkasirisha mke wa mfalme Cyrus. mwanamama huyo aliagiza jamaa kwanza atolewe macho yote bila ganzi. Akapewa dawa akapona baadae. Alivyopona ikaamuliwa achunwe ngozi mwili mzima. Akahudumiwa vizuri hadi aliopata nafuu ndio wakammalizia kwa kumsurubisha hadi kifo.
Hiyo sio mara moja. Siku nyingine wakiwa vitani mwanajeshi mmoja alipomuona mfalme amejeruhiwa akataka kumuua bila mafanikio. Mama wa mfalme akaagiza wamuache yeye mwenyewe atamshughulikia.

Kwanza alimfunga kwenye matairi mawili akavutwa pande zote nusu kugawanyika vipande viwili ambavyo bado vinaning'inia alafu akaachwa hivyohivyo siku kumi (maumivu yake ni balaa). Baadae mama huyo akamtoa macho yote mawili. Baada ya hapo alichukua Uji wa chuma unaotokota (kama umezoea maji 100C hapo ni zaidi ya 1000C) akaumimina masikioni hadi jamaa akafa kifo hicho cha tatu.
Hawa ndio wamama wa kiajemi enzi hizo ni walikuwa na roho ngumu.

3:KULIWA NA WADUDU HADI KUFA

Unaweza kudhani hii ni adhabu nyepesi sana.
Hapa ilikuwa hivi, Yule mtu ambaye alikuwa amechukiwa na mfalme. Mtesaji maalumu alichaguliwa. Mteswaji anaingizwa kwenye gome la mti kama hapo juu linalomtosha na kuzibwa chini akiwa amesimama na sehemu ya mwili wake uko njee. Ananza kunyweshwa asali na maziwa taratibu hadi atakapoanza kuharisha na gogo zima kujaa kinyesi.

(SEHEMU YA TANO)ADHABU

8:KUKATWA BAADHI YA VIUNGO NA KUWEKA MBELE YA KASRI

Hii ilikuwa ni adhabu mahususi kwa waasi (wasaliti wa mfalme), ilikuwa ukibainika tu imekula kwako, na hii ilifanyika kipindi cha mfalme DARIUS. Alichokuwa akifanya huyu mfalme ni kuagiza waasi wote wakatwe pua, masikio, ulimi pamoja na kutolewa jicho moja kila muasi, haikuishia hapo kwani walitakiwa kupelekwa mbele ya geti kuu la kasri ya mfalme ili kila mtu awaone na mtu yoyote anaruhusiwa kumpiga ili mradi asife na watahitajika kukaa hapo usiku na mchana kwa muda wa wiki Tatu, ndo anauwawa. Hii adhabu ilikuwa inatisha watu wasijaribu kumpindua mfalme.

9:KUMWAGA DHAHABU(SIO MAKINIKIA) ILIYOYEYUKA KWENYE KOO LA MTUHUMIWA

Jemedali mmoja wa kirumi aliyejulikana kwa jina la VALERIAN alipokamatwa na Wanajeshi wakiajemi alipata mwisho mgumu ambao hakuwahi kutarajia. Jemedari mmoja wa kiajemi Aliyejulikana kama Shapur 1 alimchukua kama mtumwa wake akimuamuru kutembelea miguu na mikono kama mbwa. Alipotaka kuongea alimuweka akae kama stuli kisha kukaa juu yake na kuendelea na maongezi.

Siku alipomchoka alimuua kwa kuyeyusha dhahabu (Joto lake ni zaidi ya 1000C) na kumywesha kupitia kooni ujiuji huo. Baada ya kufa alichunwa ngozi kisha kuchomwa kama mshikaki na kubaki amening'inizwa kwenye ngome ya waajemi.

Haya ndio maisha ya zamani wakati hakuna cha UN wala THE HAGUE au yoyote wa kumtetea mwenzake. Mwenye nguvu alifanya chochote alichotaka bila kufungwa na sheria yoyote. Ila pia nidahamu ilikuwa ya hali ya juu kutokana na kuwepo na adhabu hatari kama hizi....!!!! Dunia Imetoka mbali sana....!!! MWISHO....!!!!
 
Hakika ni adhabu mbaya mno ila BADO hazijafikia ile ya Bwana YESU ya kugongelewa misumari minene namna ile bila ganzi kisha kuninginizwa huku akipigwa na mijeredi.hao sijazungumzia kupachikwa taji la miiba na kisha kunyweshwa sifongo.Watu wa zamani walikuwa katili mno.
 
Hakika ni adhabu mbaya mno ila BADO hazijafikia ile ya Bwana YESU ya kugongelewa misumari minene namna ile bila ganzi kisha kuninginizwa huku akipigwa na mijeredi.hao sijazungumzia kupachikwa taji la miiba na kisha kunyweshwa sifongo.Watu wa zamani walikwa katili mno.
Adhabu ya msalaba ilikuwa in adhabu ya kifo yawarumi pia wayahudi ,ilitolewa kwa watu wengi sio Yesu peke yake wrote walio onekana waasi walitundikwa msalaban hata Petro pia aliuliwa kwa kutundikwa msalaban kichwa chini miguu juu huko rumi
 
Kichwa chini miguu juu kwakua yeye mwenyewe alisema hana hadhi ya kufa katika mkao exact kama wa Yesu.
 
Hakika ni adhabu mbaya mno ila BADO hazijafikia ile ya Bwana YESU ya kugongelewa misumari minene namna ile bila ganzi kisha kuninginizwa huku akipigwa na mijeredi.hao sijazungumzia kupachikwa taji la miiba na kisha kunyweshwa sifongo.Watu wa zamani walikuwa katili mno.
Upon Uzi nitaleta watu 10,waliokifa kwa mateso makali zaidi duniani
 
Hakika ni adhabu mbaya mno ila BADO hazijafikia ile ya Bwana YESU ya kugongelewa misumari minene namna ile bila ganzi kisha kuninginizwa huku akipigwa na mijeredi.hao sijazungumzia kupachikwa taji la miiba na kisha kunyweshwa sifongo.Watu wa zamani walikuwa katili mno.
ACHA UZWAZAZWA, KUGONGELEWA MISUMARI NA KUCHAPWA MIJELEDI sijui fimbo NAYO NI ADHABU? stori ya yesu ni ya watoto. ADHABU NDO KAMA HIZO ZA MTOA MADA.
 
Hakika ni adhabu mbaya mno ila BADO hazijafikia ile ya Bwana YESU ya kugongelewa misumari minene namna ile bila ganzi kisha kuninginizwa huku akipigwa na mijeredi.hao sijazungumzia kupachikwa taji la miiba na kisha kunyweshwa sifongo.Watu wa zamani walikuwa katili mno.
hiyo enzi hizo ndo ilikuwa kawaida sasa, mtu akihukumiwa kifo manake ilikuwa ninkusurubiwa, hivyo ni mamia pengine maelfu ya watu waliwahi kusulubiwa zama hizo, sio yesu peke ake
 
Hakika ni adhabu mbaya mno ila BADO hazijafikia ile ya Bwana YESU ya kugongelewa misumari minene namna ile bila ganzi kisha kuninginizwa huku akipigwa na mijeredi.hao sijazungumzia kupachikwa taji la miiba na kisha kunyweshwa sifongo.Watu wa zamani walikuwa katili mno.
walikuwa hawajui haki za binadamu
 
Hakika ni adhabu mbaya mno ila BADO hazijafikia ile ya Bwana YESU ya kugongelewa misumari minene namna ile bila ganzi kisha kuninginizwa huku akipigwa na mijeredi.hao sijazungumzia kupachikwa taji la miiba na kisha kunyweshwa sifongo.Watu wa zamani walikuwa katili mno.
We jamaa hebu acha utani yaani mtu kutolewa jicho upone halafu uje uchunwe ngozi unaona ni adhabu nyepesi kuliko ya bwana Yesu mihemko ikizidi ugonjwa
 
Back
Top Bottom