Adhabu ya FIFA kwa Simba na Kichuya: Namuona Kichuya kwenye mechi ya Azam dhidi ya Namungo. Adhabu ile ilifutwa ?

Mwanamaji

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2013
Posts
2,905
Reaction score
4,518
Kutokana na sakata la usajili wenye utata wa mchezaji Shiza Kichuya kutoka Misri kwenda Simba, tumeambiwa hapa juzi tu kwamba Simba ilipigwa faini ya takriban milion miatatu na mchezaji tajwa kufungiwa miezi sita.

Lakini namuona Shiza Kichuya kwenye mechi ya Namungo dhidi ya Azam hapa ameingia kuchukua nafasi ya mchezaji A. Abeid.
Wakuu kwani vipi kuhusu kale ka adhabu ketu ka FIFA ?
Kalifutwa ?
Maana miezi sita bado haijapita.

Ufafanuzi tafadhali kwa wajuvi na wajuzi.
 
Kwani siku 45 za kulipa fain zimeisha?
Kichuya alipewa adhabu ya kufungiwa (miezi 6) na sio faini.
Adhabu ya faini walipewa Simba.
Mimi nauliza juu ya uhalali wa Kichuya kucheza mechi hii wakati amefungiwa.
 
Kichuya alipewa adhabu ya kufungiwa (miezi 6) na sio faini.
Adhabu ya faini walipewa Simba.
Mimi nauliza juu ya uhalali wa Kichuya kucheza mechi hii wakati amefungiwa.
FIFA hawaja communicate formally kwa Kichuya kuhusina na adhabu waliyompa! Nadhani ndio sababu yuko uwanjani! Taarifa za Mitandaoni sio rasmi hadi mlengwa atakapo Pata barua rasmi ya kusimamishwa kwake na ukomo wa hiyo adhabu
 
Asante, nimekuelewa mkuu.
 
WACHAMBUZI VILAZA VS WASIKILIZAJI VILAZA BADO BILA BILA
 
Kichuya alipewa adhabu ya kufungiwa (miezi 6) na sio faini.
Adhabu ya faini walipewa Simba.
Mimi nauliza juu ya uhalali wa Kichuya kucheza mechi hii wakati amefungiwa.
Wewe ulisikia wapi?
 
Taarifa za mitandaoni tunazivumisha sana bila ya kujua huku mitandaoni ndio kuna hadi signature ya Rais
 
Ishu ya kichuya Simba wameomba mapitio ya kesi yao, kwahiyo wakiomba hivyo ina maana maamuzi yanasimama,kwahiyo Kichuya anaendelea kucheza mpaka maamuzi tena yatakapotolewa ya mapitio ya kesi
 
Vipi barua hiyo ilitaarifu namna ya usajili ulivyofanyika au kuzuiliwa kwa kichuya?
Kama barua ilifika Namungo obvious ni lazima iwe inaelezea adhabu ya Kichuya, Vinginevyo isingeenda Namungo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…