Adhabu ya kufukuzwa shule ibadilishwe

Adhabu ya kufukuzwa shule ibadilishwe

Mkoba wa Mama

JF-Expert Member
Joined
May 5, 2021
Posts
208
Reaction score
91
Taifa linahitaji vijana wasomi na wenye elimu na maarifa ya kutosha, sasa inakuaje tena kunakuwa na adhabu ya kuwafukuza shule vijana hawa ambao ndio taifa la kesho pale wanapokutwa na makosa ya utovu wa nidhamu wakiwa shule wakitafuta elimu ambayo ndio mkombozi wao wa baadae?

Unamfukuza shule ili aende wapi? Na kumfukuza shule ndio kumfundisha nidhamu? Na baada ya kumfukuza shule anabaki kuwa mzigo wa nani? Na Je, umemuandalia mazingira yapi baada ya kumfukuza shule? Ni baadhi ya maswali machache ambayo tunapaswa kujiuliza.

Ingefaa zaidi adhabu hii iondolewe na kuwepo na adhabu mbadala kama vile kazi za mikono, kukariri mwaka wa masomo au mwanafunzi anapokutwa na kosa apelekwe JKT kwa mda fulani hata mwezi mmoja akafundishwe nidhamu huko na sio kumfukuza shule.

Adhabu ya kuwafukuza shule niya kikatili inayokatisha ndoto za vijana wengi, kuharibu maisha yao ya baadae na ishara ya wazi kabisa ya udhaifu mkubwa wa serikali kwa kushindwa kuwalinda vijana wake ambao ndio taifa la kesho na kuwatelekeza kikatili huku ikiwanyima haki yao ya msingi ya kupata elimu, lakini pia hii ni kuendelea kujikaanga wenyewe na kuendelea kutengeneza taifa la wajinga wengi wasio na elimu, na ujinga ndio msingi mkuu wa matatizo mengi katika jamii zetu.

Serikali na wizara husika mlitazazme suala hili upya na kwa upana wake.
 
Ni jukumu letu kama wazazi/walezi kuwalea watoto wetu katika maadili mema pia kuwazoea utii wa sheria bila shuruti hii si tu itawasaidia kuepukana na adhabu kama hiyo ya kufukuzwa shule/vyuo lakini pia itawaweka mbali na matatizo yasiyo ya lazima.
 
Back
Top Bottom