"Why do we Kill People who Kill People to Show that Killing People is Wrong ?"
Je ni sawa kuwa na Hukumu ya Kifo?
Baada ya yule Chizi wa Norway kuua kadamnasi ya watu (ukizingatia Norway life Sentence ni limited kwa miaka 21 tu) Je ni muhimu kuwa na hukumu ya kifo? Ni nini hasa faida ya hukumu ya kifo?
Je hukumu ya kifo inafanya watu waogope kutenda maovu kwahiyo ni njia nzuri au ni kuonyesha hata sisi hatuna tofauti na waliofanya hayo maovu?
I can argue kwamba huenda hukumu ya kifo ni adhabu rahisi sababu badala ya kumfanya mtu ku-suffer kwa kosa lake, tunampumzisha. Je sio vema kumfunga mtu maisha na kumfanyisha kazi ngumu kwa maisha yake yaliyobaki na kila alichonacho au atakachokitengeneza kiende kwa wale aliowatenda?
Sheria haiwezi kupitwa na wakati bali watu ndo ndo wanaopitwa na wakati wanatunga sheria zinazoweza kuwabeba au kuifanya jamii iwe zembe! Sheria ni nzuri cha msingi ni wether mtu alifanya makusudi au kasingiziwa? Kwa sababu kwenye jamii kuna vichaa wanawaza kuua watu Kama majambazi utakuta mtu mwizi mdogo tu anafanya armed robbery anaua kisa anavizia kaduka kadogo! Kazi ya sheria ni kudhibiti vitendo viovu na au watu waovu.
What do you think?