Adhabu ya viboko, imekuwa unyanyasaji kwa wanafunzi Tanzania

Adhabu ya viboko, imekuwa unyanyasaji kwa wanafunzi Tanzania

Ngida1

JF-Expert Member
Joined
Aug 25, 2009
Posts
586
Reaction score
206


Jamani, nimeiona video moja kwenye YouTube kwa kweli inatia haya kwa walimu wa nchi hii ambao ni wachapa kazi. Katika video hio inaoneshwa Mwalimu Mkuu wa kike anawapiga watoto bakora kama vile yeye mwenyewe hajazaliwa.

Haya mambo ya kuwapiga sana watoto mpaka tukawafanya masugu kwa kweli sio mazuri hata kidogo. Bakora au fimbo hailei wala haisomeshi, bali inaharibu tu. Walimu punguzeni kupiga watoto na somesheni zaidi madarasani!

Sisemi kama watoto wasitiwe adabu, lakini adabu ilingane na umri wa mtoto na iwe ya kiasi. Sio mwalimu anapiga tu kisa mtoto hajui hesabu!
Kama huyu mtoto ni mwanangu basi huyu mwalimu tungelitambuana vizuri sana vichochoroni !

Tuwaoneeni huruma watoto wetu! Itafute hii video kwenye YouTube chini ya maneno hayo yaliopo kwenye title ya msg hii, ili ujionee mwenyewe walimu wetu wanavyofanya unyama kwa watoto wetu mpaka wageni wanaiomba serikali yetu ichukuwe hatua kwa walimu kama hawa. Hii ni aibu kwa sote hapa Tanzania.
 
Last edited by a moderator:
Wewe naona umekosa kazi. Kuchwapwa huku ndio unaona ubaya? Kuna watoto wengine hawaelewi maana ya elimu hadi wachapwe. Huyu mwalimu hajamwadhibu mtoto vibaya. Amemchapa kwenye mat.ako na hatumiii fimbo, bali yuatumia kijiti. Tayari nishairipoti video hii kwa you tube kwa kuwa haina nia yoyote ila kuwachafulia walimu jina.
 
MwendaOmo Mwanafunzi huyo anaadhibiwa bila kosa, na adhabu yake haiwezi kumsaidia chochote, kwanza mwanafunzi kufeli makosa ya mwalimu na mwanafunzi ni 50 kwa 50. Hapo nani anatoa adhabu kwa makosa yanayofanywa na mwalimu ? sikiliza kauli ya mwalimu, anasema mwanafunzi alivyofeli amemdhalilisha, badala aumize kichwa mbinu mbadala za kumfanya aelewe yeye anakimbilia kuchapa, Hakuna taaluma hapo ni uchizi tu.
 
Ndugu MwendaOmo, kwa kweli unatusikitisha wengi kwa huu msimamo wako ambao ni wa Century ya 5 nyuma. Hatusemi mtoto asichapwe au asitiwe adhabu kwa makosa, lakini adhabu iwe sawa na kosa. Kama mtoto hajui hesabu, tafadhali asaidiwe na kama hataki kusaidiwa hapo tena atiwe adabu kidogo na sio viboko 8 kama alivyovipata yule mtoto. Unadhania yule mtoto karejea tena darasani au kaenda kwao kuchunga ng'ombe? Tafadhali, kama ni mwanaadamu yule mtoto,fikiria na vile alivyodhalilishwa pia!
Ndugu MwenadaOmo, umemsahau yule mtoto aliyepigwa na mwalimu mpaka aka-paralyse? Ndio kweli unataka kuwapa walimu licence ya kuwa-paralyse watoto wetu kila siku?
Badala ya kuwapiga watoto kwa kufeli, ilibidi yule Mwalimu Mkuu awatie bakora walimu wa wale watoto kwa kukosa kuifanya kazi yao inayowapa riziki kama vile inavyotakiwa!
Jamani, tusiwape nguvu walimu wakawa kama ma-Dictator fulani maskulini mwetu. Tukifanya hivyo tutaelekea pabaya kama nchi!
 
Ukitaka umpoteze moja kwa moja mtoto wa kitanzania, basi usimpe adhabu ya viboko.

Physical punishments zina cost sana ktk upande wa mda kwa mwanafunzi na mwalim, hivyo atapeteza mda mwingi sana wa kujisomea.

Psychological punishment, ukiitumia, utamuua mtoto maisha yake yote.
 
Ndugu Dzudzuku,

>Ukitaka umpoteze moja kwa moja mtoto wa kitanzania, basi usimpe adhabu ya viboko.
Inamaana yale maneno kuwa punda haendi mpaka kwa bakora ni kweli kwa mtoto wa kitanzania?

>Psychological punishment
Hakuna anaependekeza psychological punishment. Hii ni mbaya zaidi kuliko hivyo viboko!

Simply, tuwe wastaarabu na tuwasomeshe watoto wetu kama ipasavyo kwa ustaarabu na sio kwa ujangiri kama wa yule headmistress. Huko kote ambako hawatumii corporal punishment mashuleni mbona ndiko ziliopo successful societies leo? Huku kuwa na roho za ukatili ndiko kunakoturejesha nyuma na kutuharibia maendeleo yetu.
Mtoto aliekuwa keshazowea kupigwa hatoogopa kuchota kutoka escrow account. After all adabu gani atapat zaidi ya viboko alivyokuwa keshavizowea tangu enzi za shule?


 
shule bila viboko taaluma ya wanafunz inaweza kushuka kwani watahitaj kufanya mambo kwa matakwa yao,nikupe mfano mimi mwenyewe primary hasa darasa la sita nilikuwa mtukutu kinoma mpaka nilitaka kutoendelea na shule ila mama yangu mzaz na walimu hawakukubali,kila siku home viboko shule viboko mpaka nikafuata taratibu za shule na kuacha ujeur shulen,viboko vilinifanya nifaulu primary kwenda sekondary,kule nilitaka kufuata mikumbo mibaya nikanyoshwa viboko vilivyo kilasiku tena vya maana niliona wananitesa ila nikabadilika moja kwa moja,nikafaulu poa 2010 na kwenda advance level mkoan njombe na sasa nipo chuo kikuu cha MKWAWA IRINGA-TOWN ila viboko viwechangia sana kufaulu kwangu kwa asilimia kama 70%
 
adhab inatokan na mazingira , haya mambo ya kuparamia et haki za mtoto ni kuharib misingi ya makuzi ya mtot wa kiswahil ndiyo maana hat leo hii ukipand daldal utamkut mtot wa shule kakaa kwa kiti na mtu kama babu au bibi ake amesimama....mbona wao hawaigi tamaduni zetu ?

maandik yenyew yanasema ,bakora kwa mtot na mjered kwa faras...
 
shule bila viboko taaluma ya wanafunz inaweza kushuka kwani watahitaj kufanya mambo kwa matakwa yao,nikupe mfano mimi mwenyewe primary hasa darasa la sita nilikuwa mtukutu kinoma mpaka nilitaka kutoendelea na shule ila mama yangu mzaz na walimu hawakukubali,kila siku home viboko shule viboko mpaka nikafuata taratibu za shule na kuacha ujeur shulen,viboko vilinifanya nifaulu primary kwenda sekondary,kule nilitaka kufuata mikumbo mibaya nikanyoshwa viboko vilivyo kilasiku tena vya maana niliona wananitesa ila nikabadilika moja kwa moja,nikafaulu poa 2010 na kwenda advance level mkoan njombe na sasa nipo chuo kikuu cha MKWAWA IRINGA-TOWN ila viboko viwechangia sana kufaulu kwangu kwa asilimia kama 70%

nafkiri bado unahitaji viboko kwa ajili ya maendeleo ya maisha yako,,,
 
Back
Top Bottom