Ngida1
JF-Expert Member
- Aug 25, 2009
- 586
- 206
Haya mambo ya kuwapiga sana watoto mpaka tukawafanya masugu kwa kweli sio mazuri hata kidogo. Bakora au fimbo hailei wala haisomeshi, bali inaharibu tu. Walimu punguzeni kupiga watoto na somesheni zaidi madarasani!
Sisemi kama watoto wasitiwe adabu, lakini adabu ilingane na umri wa mtoto na iwe ya kiasi. Sio mwalimu anapiga tu kisa mtoto hajui hesabu!
Kama huyu mtoto ni mwanangu basi huyu mwalimu tungelitambuana vizuri sana vichochoroni !
Tuwaoneeni huruma watoto wetu! Itafute hii video kwenye YouTube chini ya maneno hayo yaliopo kwenye title ya msg hii, ili ujionee mwenyewe walimu wetu wanavyofanya unyama kwa watoto wetu mpaka wageni wanaiomba serikali yetu ichukuwe hatua kwa walimu kama hawa. Hii ni aibu kwa sote hapa Tanzania.
Last edited by a moderator: