ni muda mrefu sasa wanaharakati mbali mbali wamekuwa wakipigia kelele swala hili. Nchi kadhaa duniani ikiwemo kenya wamefuta adhabu hii.kwao hii ni jinai;mwalimu au mzazi ukibainika amemchapa mtoto unawajibishwa.hapa tanzania adhabu hii bado ipo,ila kuna utaratibu na kikomo cha kuitoa hasa shuleni.
Swali:kwa mazingira yetu haya,je umefika muda muafaka wa kuiondoa kabisa adhabu hii nyumbani na shuleni? Kama tunataka iendelee je,utumike utaratibu gani wa kuitoa hasa nyumbani?
Kudesa(kuiga) kila kitu bila kuangalia mazingira ndo kinachotusumbua watanzania, kwa vile wazungu hawachapi na sisi tusichape, tuko tofauti sana nao kimaadili na kila kitu, watoto wetu lazma wapate kiboko lakini kwa kiwango stahiki na kwa utaratibu bila jaziba.
ni muda mrefu sasa wanaharakati mbali mbali wamekuwa wakipigia kelele swala hili. Nchi kadhaa duniani ikiwemo kenya wamefuta adhabu hii.kwao hii ni jinai;mwalimu au mzazi ukibainika amemchapa mtoto unawajibishwa.hapa tanzania adhabu hii bado ipo,ila kuna utaratibu na kikomo cha kuitoa hasa shuleni.
Swali:kwa mazingira yetu haya,je umefika muda muafaka wa kuiondoa kabisa adhabu hii nyumbani na shuleni? Kama tunataka iendelee je,utumike utaratibu gani wa kuitoa hasa nyumbani?
Kwa taarifa yako hata hiyo adhabu ya viboko Tanzania walileta wazungu, ndio waliotufundisha kuchapa watoto, yaani jinsi wanavyochapwa leo shuleni, matakoni au mikononi na ni viboko vingapi vinaruhusiwa hayo yote walileta wazungu, na walileta kutoka kwao kwa maana wakati huo hata wao pia watoto wao walikuwa wanachapwa shuleni, lakini sasa hivi hawachapi watoto wao tena kwa maana wameshapima na kujiuliza maswali mengi sana pamoja na hayo unayojiuliza wewe na wakagundua kuwa kumchapa mtoto hakumsaidii chochote katika maendeleo yake ya kitaaluma na kimaisha wakaamua kufuta, sasa kwa nini na sisi tusifute, kama waliotufundisha kuchapa hawachapi tena?